Author :
Anonymous-37
Date:
Sun, 17 Dec. 2000
Subject:
TUMEFANYA NINI?
From: Anonymous-37
Subject: TUMEFANYA NINI?
Asalama Alaykum Wote,
Sk. Mohammed bin Juma (my-ex-schoolmate) natumai hujambo.
Habari za siku nyingi, na habari za Paris, vipi hali ya hewa ya huko.
Swali lako zuri sana, ulilouliza juu ya mada "Fix it" Diplomacy.
Kabla ya kuendelea na jawabu, nitapenda kukuliza swali kidogo Sk. Mohammed.
Je, mpaka sasa hujaona Wazanzibari wamefanya Nini?
Sasa tuendelee. Sk. Mohammed na wengine wote wana-ukumbi wetu adhimu.
Nitapenda kulidahili swali hili kwa jawabu zifuatazo:
i. Wazanzibari tumefanya mengi: Tumeweza kuupigia VOTI ya NO utawala wa CCM
mwaka 1995 na 2000. Lakini CCM haikubali kutoa nchi. Sijui kwa mazingira
kama hayo, tufanye NINI zaidi ya "kupiga kura".
Hatuwezi kumtoa Amani ndani ya Ikulu, hatujafikia bado kuingia barabarani.
Kwa nini? Hatuwezi kugaragara barabarani, na kudai Haki yetu/zetu
(1995/2000) tulizonyanganywa na CCM kwa nguvu. Sijui kama ni sahihi kufanya
hivyo, kwa wakati huu....
- Jeshi/Polisi/vyombo vya Dola bado vina-uadilifu mkubwa kwa Serikali.
Tofauti na Yugoslavia, kuwa vyombo vya dola, vilikuwa na upinzani.
- Lakini, walikuwa hawawezi wao kuanza "ngoma", walisubiri Upinzani uanze
kupiga chapua/halindwa, na wao waanze kucheza (See interview ya Kostunika,
by John Simpson, BBC).
ii. Wazanzibari, mwaka 1999, walifanya jambo kubwa sana - Kuukataa mfumo wa
Muungano wa Serikali mbili, kikatiba na sheria - kupitia Maoni ya White
Paper Commission. Ilikuwa dalili nzuri ya kuwapa credit, na kuona kuwa
"tumechoka".
iii. Wazanzibari, kwa nafsi zao, bayana yao, na upendo wao kwa nchi yao -
watu wao, waliupokea Muwafaka baina ya CCM-CUF, kwa roho safi kabisa. Hapo
ilikuwa njia moja ya kufahamiana zaidi, kuondosha uhasama na ufisadi
uliopandikizwa na CCM ndani ya jamii ya Zanzibar.
Hatimaye kupata Maslahi ya Zanzibar, kwa njia za salama, na taratibu - Kwa
murua!
iv. Achilia hayo ya hivi karibuni: Rudi nyuma kidogo kati-kati ya 80s , uone
patashika ndani ya CCM, Wazanzibari walivyochachamaa ndani ya CCM, kutaka
NCHI yao.
v. Wazanzibari wengi wamepinga kuwepo wale mafisadi wa ZEC - Tume ya
Uchaguzi. Lakini kama nilivyowahi kusema huko nyuma, Zanzibar sio Columbia,
au El-Salvado. Ingalikuwa hivyo, maudhi ya watu kama hawa (ZEC) ni rahisi
sana "kukabiliana" nao.
- Lakini misingi ya Imani yetu, hasa ya dini, utu wetu, busara zetu, hisia
zetu, heshima zetu, hairuhusu kufika huko.
- Kigezo hicho, pia ndio kinatumika kama "udhaifu" wetu na akina Stith na
Maliyamkono kufanya wanavyotaka.
va. Hapo tulipata kundi la akina Seif and CO Ltd. Kabla ulikuwa na akina
Ramadhan haji Faki (1+1 = 3).
Utakumbuka, hata tulipokuwa skuli, tulikuwa tukiona na kuunga mkono
Mapambano hayo.
Kwa fikra zangu mimi (pengine ni wrong), naona hizo zote ni moja ya juhudi
za Wazanzibari kutaka kujikomboa, au kufikiria kujenga misingi mizuri ya
haki, na uadilifu katika jamii yetu (social justices).
Swali: Nitaomba nikuulize swali jengine (kumradhi kwa maswali mengi). Je,
Nini vigezo vyetu vya kujua Tumefanya Nini, na tunachotakiwa kufanya NINI?
2. Tuendelee na mada yetu. Ama Sk. Mohammed na wenyeji wa barza hii, kama
tutasema kuwa: Wapo Wazanzibari miongoni mwetu wanaotufisidi, hiyo
ninakubaliana na mtu yeyote 100%.
Kwa mfano, hayo anayoyasema Stith na wenzake, ujue kuwa kuna Wazanzibari
(wengine ni wenzetu kwa njia moja au nyengine katika net hii), wamehusika
katika "kumlisha" fikra hiyo, na kuamini hivyo.
Ni kweli, baadhi ya Wazanzibari ndio wanaoisalaiti nchi yetu, kwa hali na
mali. Utakumbuka Sk. Mohammed, kuna Wazanzibari, walibuni ma-documents ya
uwongo, na kukifananiza CUF, kama ni Chama cha waislamu? Na Documents hizo,
kwanza, zilipelekwa Ubalozi wa Marekani, DSM. Walichukua fikra, eti CUF
kina-base yake huko Southern Sudan.
** Angalia, Southern Sudan sio Waislamu, ni akina John Garang? Uhusiano huo
vipi? Mara Waislamu, mara Southern Sudan!
Sk. Mohammed, na wenzetu wote, hayo yamefanywa na Wazanzibari, halisa, "kina
bin kinana-na nani-hiliya!".
Tufahamu kuwa, wakati mimi/wewe, tunajenga, wenzetu wengine, wanavunja, na
kuiporomosha nyumba chini kwa bulldozer.
ii. Chukua mfano mwengine, ZEC: Sijui ni tija gani, na maslahi gani kimaisha
watu kama ZEC, wamefanikiwa, wakati wanapoendelea kuihujumu Zanzibar, kwa
miaka kumi mfululizo sasa.
Kama hawa, tuwaingize katika kaumu gani? Wazanzibari, tumepinga himaya ya
ZEC, mimi binafsi Allah ndiye ajuaye, namna gani moyo/nafsi yangu iko juu ya
watu hawa. Hawa tunaambiwa eti ni Waislamu. Mimi siamini hivyo.
iii. Tuangalie Dr. Omar na Muungano wake. Tumesoma habari kuwa Dr. Omar
anashauri kuwa "maoni ya Muungano ya 1994, ndio yafuatwe".
a. Kwa taarifa yako, maoni haya yalipingwa na SMZ, yenyewe, na Dr. Omar
binafsi ofisi yake ndio iliyokuwa ikisimamia maoni haya, na kuonyesha
kutoridhika nayo.
b. Maoni haya, ndio yanaondosha passport, Uraia wa Zanzibar, U-rais wa
Zanzibar (somehow), na hata kuiondoshea Zanzibar hadhi/heshima ya kukusanya
kodi. Kwa ufupi, hii ndio Shelukindo Report
** Angalia, huyu ni Mzanzibari, na anataka tufuate ripoti hii. WHY?
Kwa lugha ya mkato, anataka tuizike Zanzibar, jumla jamala, na hitma
itafanyika Msasani!
c. Kuna ripoti ya White Paper, ambayo hasa ndio maoni ya Wazanzibari,
wanavyotaka, Dr. Omar, amerukia sio matawi, bali vilele vya mti, na kuacha
shinda. Ameacha ripoti ya 1994, na kufufua "historia" ya 1994.
Kwa hali kama hiyo, Wazanzibari wa kawaida, si rahisi kuweza kupambana nayo.
Sijui wenzangu. Maana, kila tukitaka kuezeka paa, basi wengine wanaivunja
nyumba kuanzia msingi.
Pamoja na hayo, hatukulala, bora tunaishi, uhai, uzima upo, basi tutaendelea
tu, kudai haki yetu.
Inasemekana Mayahudi, ilichukua miaka 2000, eti kupata nchi yao, East Timor
imechukua kama miaka miaka 20...Ukraine and other ex-Soviet states,
imechukua zaidi miaka 50 n.k.
Sijui Zanzibar, tutachukua muda gani. Hapana shaka yeyote, miaka 37, sasa
inakatika bila mafanikio makubwa, lakini bado OUR SPIRIT IS ALIVE.
Falestina, mpaka sasa wanadai nchi yao: wao wanapigana kwa mawe, au panda na
Israel. Basque State, pia wanapambana kudai nchi yao--tusikate tamaa Sk.
Mohammed.
Sk. Mohammed, na wengio wote, kwa taarifa niliyopata hivi karibuni (kutoka
kwa ndugu yetu mmoja), amenidokeza kuwa mpaka sasa, State Department, na
Idara nyengine, hawana hasa taarifa kamili juu ya NINI kinaendelea Zanzibar
- ukorofi wa CCM, unyama wa polisi, na hujuma za uchaguzi.
Wanategemea zaidi, ubalozi wa Tanzania, Washington (Haya! paka unamuwekea
samaki?. Tusisahau pia mfumo wa Uendeshaji wa Idara kama hii ni Urasimu
zaidi.
Kwa maana hiyo, bado tunaweza kuwa na nafasi nzuri ama ya kutoa taarifa
zilizo sahihi zaidi, au hata kutengeneza "Civil petition" ya mustakabli wa
mambo yetu.
Ni kweli, Idara kama hiyo ina Urasimu wake, na inafanya kazi, katika mifumo
ya kijasusi zaidi, hivyo kila kitu kinatiliwa shaka, na khofu.
Tuendelee kupeleka, kila pahala, kila tunapoona panahitajika kufahamishwa --
information is power! Kumbuka kuwa Hitler alikuwa anamini kuwa "kusema
uwongo mia moja", basi inabadilika kuwa kweli".
Tuendelee kuonyesha kuchukiwa na hayo yaliyofanyika, na yanayofanyika
Zanzibar.
Iko siku watakuja kuona ukweli, na kuamini tu. Lakini, na sisi, tuonyoshe
bayana, na hisia zetu kwa Zanzibar. Sk. Mohammed, inshallah nakutakia masomo
na mafanikio mema katika maisha - Amen.
Inshallah, nakutakieni Ramadhan Njema - Amen.
Wako Mtiifu katika Kazi,
NO-37