Author :Dr. Thurayya Cahill
    Date:Sun, 21 Dec 99
Subject: UGONJWA WA KISUKARI
_____________________________________________________
     
Assalaam Aleykum wanazanzinet,

Assalamu Alaykum Dr. Omar, Dr. Yussuf, Sheikh Issa na wananeti,

Nimo kwenye likizo basi nimepata nafasi ya kuandika na kufuatilizia habari. Furaha ilioje kwa kuona mazungumzo ya ugonjwa wa sukari. Maelezo ya ugonjwa huu ni makubwa na kama alivyosema Dr. Omar hayataki pupa na ni muhimu yaelezwe vizuri na yafahamike. Kumeulizwa suala juu ya vipimo vya sukari. Suala hili linaulizwa sana nawatumiaji wa mashini mbali mbali. Kama alivyojibu Dr. Omar inategemea mashini ya mtu. Mgonjwa lazima aifahamu mashini yake na ajaribu kufahamu kwa nini anapata vipimo mbali mbali.

Maradhi ya sukari hayana utibabu lakini yanaweza kua controlled (kudhibitiwa) vizuri khasa mtu akiaangalia chakula chake, akatumia insulin (insulin dependent patients) anavyoelekezwa na akajaribu kuweka balance ya sukari mwilini sawa. Mwenye ugonjwa wa sukari anataka aweke balance baina hypoglycaemia (Low blood glucose)na hyperglycaemia (High blood glucose). Good control ya sukari ni kuhakikisha kua kipimo cha sukari hakiko chini sana wala juu sana. Maradhi ya sukari yanaleta athari nyingi mwilini kama macho, mafigo, strokes. Sasa haya yote tunaweza kuyapunguza na kuyaondoa in certain cases kwa kuangalia siha zetu.

Nasaha:

- Wagonjwa wa sukari tafadhalini fwateni maamrisho mnayopewa kutoka spitali.

- Msichanganyishe madawa ya kienyeji na ya hospitali. Ama tumieni ya spitali au ya kinyumbani tujue ipi inakufaeni zaidi.

- Research yangu inaonyesha kua wagonjwa wanachanganisha madawa ya kienyeji na ya kispitali. Hapa pana problem kubwa ya wagonjwa kutofata maamrisho ya hospitali ikisha wanarudi na kunungunika.

- Kuna wagonjwa wa sukari wanoamini kua wakila chochote kile cha sukari halafu wakala muru, shubiri, korela au kitu kichungu basi haidhuru. Utasikia kua ukisha kula kitu kichungu basi sukari inateremka. Ndio kisomo chako kinaonyesha kua sukari imeshuka lakini haina maana kua ugonjwa wa sukari huna tena. Hii shubiri inonywewa baada ya kula vitu vya sukari ina mashakil yake pia. Kwa wagonjwa wengine huwaharisha sana na wengine inaharibu matumbo.

- Watumiaji wa insulin kwa hisani zenu tumieni insulin zenu sawa sawa. Ikiwa mwili haufanyi insulin basi korella hazifai. Hii miti shamba huweza kufanya kazi kwa watu wenye type 2 diabetes and mild forms of the illness.

Sheikh Issa umezungumza kuhusu miti shamba. Mie mwaka huu nimemaliza research kuangalia uhusiano wa afya na utumizi wa miti shamba. Hili ni buku ambalo litakua published mwakani inshaalla. Research hii inaendelea kutizama dawa za kienyeji zinazotumiwa kwenye maradhi ya sukari, pumu na dhoofu ya damu. Sasa hapa tutafanya intervention study ya kutizama uwezo wa dawa hizi kusaidia magonjwa haya. Hizo institute ulizozitaja ziko nyingi lakini panahitajika research zaidi. Bila ya research sawa sawa hakuna credibility. Lakini pia idea yako naiunga mkono.

Research yangu inatumiwa katika kusomesha health professionals hapa na nikisha kupublish inshaalla na kwengine. Kuna mwenzangu humu aliniuliza privately nimletee training programme tunotumia hapa katika non-communicable illnesses, khasa diabetes. Programma hii nitaitia humu ukumbini kwa faida ya wote.

Dr. Yussuf idea yako nzuri sana lakini mie naona bora masuala yaulizwe humu hadharani kwa sababu nakumbuka nyuma kidogo nilikua nikipata masuala mengi ambayo wewe umeshayataja. Mushkil ulikua atakuja mwengine atauliza suala lile lile. Wakati ukilijibu suala hadharani wengi watasikia. Wacha watu wewe wakuletee masuala yao lakini wewe wajibu hadharani kwa faida ya wote bila ya kutaja jina la muulizaji.

Fikra yako ya kutafsiri maneno kwa kiswahili nakubaliana na wewe. Mwaka huu pia nachapisha vitabu vya health training kuhusu 'psychological aspects of care'; 'culture ethnicity and care'. Kazi hii inatokana na research yangu na nimeombwa na Health Service ya hapa niwaandikie vitabu hivi kuhusu professional training. Nataraji kuvichapisha kwa kiswahili pia. Hii ni kazi yangu binafsi.

Dr. Yussuf unaonaje kuhusu kuandika kitabu kuhusu huu ugonjwa wa sukari kwa kiswahili. Kitabu kidogo tu cha kufahamisha vizuri kuhusu ugonjwa huu na khasa nini kinatokea mwilini na vipi kujiangalia kisiha kwa mwenye ugonjwa huu. Inataka tutie vipicha hivi vya kusaidia maelezo. Haina haja hata ya kumcharge tu. Tufanye kwa nia ya kusaidia. Ugonjwa wa sukari tufahamu kua unawahusu familiy nzima na sio mgonjwa tu. Ugonjwa huu una psychosocial basis kama unavyojua. Ni bora familiy nzima wafuate mwendo mzuri wa kula na kumsaidia mgonjwa khasa mgonjwa akiwa mtoto. It's not a matter of educating the patient but the whole family. This is the way forward.

Ndugu yenu,
Thurayya

 Mail Comments to :Dr. Thurayya Cahill

Maintained by rai@ee.bilkent.edu.tr