Author :Abdullah Abdullah
    Date:Fri, 31 Dec 1999
Subject: 1963, Jee utafika Ramadhan nyengine wewe bado uko hai?
_____________________________________________________
     
Assalaam Aleykum waneti,

kwanza nianze kwa ramadhan mubarak na kwa niaba yangu na waliokaribu yangu pia naomba kukutumieni salamu za Iddi Mubarak na pia Mwaka mpya na mellenium, na karne mpya.

Pia naomba nichukue hii fursa kukumbusheni wananeti kuwa kadri siku zinavyopita na maisha yetu yanakatika na kabiri tunazisogelea kwa nguvu sana. Kwa hiyo, tafadhalini ndugu zetu kwa ihsani zenu na Mola wenu alizokufanyieni, tafadhalini sana tuzitumie hizi siku za mwisho wa ramadhan kwa kujiwekea hakiba ya safari yetu ngumu ianzayo kaburini na kuendelea.

Ni hasara kubwa kwa mwuislam kuwa bado yuko macho usiku wa saa saba au nane na akalala bila ya kusali hata rakaa mbili. au akautumia usiku wake kwa michezo kama karata au games badala ya kusali na kujiombea dua yeye na wazee wake.

mtu yeyote ataziachia siku hizi tukufu zukampita bure basi for sure atajuta na sana baadae. bila ya shaka atayezitumia vizuri ni hahika kuwa hatojuta hapa duniani wala akhera. Ikiwa unajihisi huna nafasi au ni mvivu basi kumbuka siku ambayo watu watajumuika pamoja kukupeleka katika malazi yako ya muda usiojulikana ndugu yangu halafu uamue jee utacheza au kustarehe na usingizi au huu wakati wa mavuno utautumia vizuri.

Amma hakika atayefanya mazuri hayo ni yake na yatamfaa mwenyewe, na atayefanya kinyume chake basi ahakikishe kuwa he/she will pay the price. Hii ifanye kama ni Ramadhani yako ya mwisho kwani hakuna aliyena hakika kuwa atafika Ramadhani ijayo. Jee ndugu yangu umefanya nini wewe katika Ramadhani hiii? ikiwa hujafanya basi fursa bado unayo, sali sana usiku, omba dua nyingi, soma sana Quraaan angalau dakika tano baada ya kusali kila sala.n.k.

Naona nisimame hapo, wa billahi taufq.
Abdullah.

 Mail Comments to :Abdullah Abdullah

Maintained by rai@ee.bilkent.edu.tr