Author :
Abdullah Abdullah
Date:
Tue, 08 Feb 2000
Subject:
NCHI YETU, ZANZIBAR
Asslaaam alikum Wananeti.
Mimi ni mzanzibar ambaye sina cha kuchangia katika neti hii iliyojaa wasomi
lakini kwa leo nawaomba kwa ihsani zenu mnisikilize.
Kila mtu anaelewa mambo yanavyokwenda nyumbani kwetu zanzibar na pengine
kuna watu wengi wenye fikra kama zangu kuhusu matokeo ya ugomvi wa
Wazanzibari na fursa inavyotumiwa na wenye mipango yao dhidi ya Wazanzibari.
Bila ya shaka ndugu zangu mko macho, lakini nahisi kutokana na mambo
yaliyotuzunguka hivi sasa tuwe macho zaidi. tabia yetu ya kugombana kwa
maslahi ya kibinafsi tuiache kwani nchi yetu inatutoka na hali tunajuwa na
tunaiona ikiondoka. bahati mbaya ni kuwa kila wazanzibari tunapotokea
kutofahamiana wenzetu wa bara huchukuwa fursa ya kupitisha miswada yao
amabayo pengine ina faida ya muda mfupi lakini huwa ni kensa kwa nchi ya
zanzibari na pale tunapokuja kuamka huwa tayari tumeshajifunga kwa sheria
ambazo tumezipitisha wenyewe bungeni.
Mwaka 94/95 ilipitishwa mapendekezo bungeni ambayo yalimfanya Rais wetu wa
zanzibar kuwa sio tena Makamo wa rais tanzania, Kwa nini?
hivi sasa kutokana na magazeti yasemavyo ni kuwa Rais wetu ni wa Nne
kimadaraka ya Kitanzania. Jee hatukujuwa haya Wazanzibari? Jee ni kwa
manufaa ya nani mapendekezo hayo yalipopitishwa? Jee nini matokeo yake hivi
sasa? Rasi wetu amabye ilikuwa awe wa Pili kimadaraka Katika Jamhuri ya
Muungano sasa anapotaka kutowa uamuzi imekuwa hauna nguvu kama Kiongozi
Mshirika wa Jamhuri hii. Jee Mwenyekiti wa CCM hawezi kumuuzulu Rais wa
zanzibar kama Mwanachama? Ikiwa anaweza jee tunasahau mambo kama hayo.
Hivi sasa mapendekezo na miswada mipya imekuja tena baada ya kuhisi kuwa
wabunge wetu wa CCM zanzibar hawana la kuchaguwa ila kuyakubali mapendekezo
hayo huko Bara pengine ili na wao waachiwe bila pressure kufanya mabadiliko
huku nyumbani pia. Lakini jee ikiwa itatokea hivyo, ni nani atayekuwa
mshindi na nani atayepata hasara ya milele. bila ya shaka ni Wazanzibari wa
makunduchi, Chaani, Micheweni, Chake chake, Matemwe,Mzambarauni,Tumbe,
Tumbatu na kwengineko. Jamani kwa ihsani zenu fikirieni mapinduzi yalifanywa
kwa damu nyingi kupotea na roho za Waislam kwa lengo la kutafuta kuondowa
madhila, uonevu, dharau, na kuwa kila mzanzibari awe huru na haki nchini
kwake.Jee haya mapendekezo tunayoyapitisha Bungeni kila mara bila ya
kupingwa na wazanzibari yatawaletea au kuwadumishia wazanzibari uhuru wao,
yataondowa au yataleta tena madhila? Jee dharau haitomfika tena mwafrika
Mzazibari jamani? Jee madhila hayatorejea karibuni jamani? Jee uhuru wetu
kama Wazanziari bado tunao? Jee tunao uhuru wa kuhjiamulia ndugu zangu?
Sasa ikiwa tuko tayari kupitisha kila pendekezo linaloletwa bungeni ili
tuendelee kupata pesa za ubunge au kuogopa kusema kweli basi ndugu zangu
Wazanzibari tujutayarishe kuwa vizazi vyetu vijavyo havitokuwa na nchi,
uongozi, pahala pa kujidai kusema hapa ni kwetu.
ndugu zangu wazanzibari, leo wanaoathirika na hali ya kisiasa zanzibar ni
Wapemba lakini kwa namna miswada munavyoikubali bungeni ipo hatari kwa kiasi
kikubwa kuwa na Wazanzibari asilia watafikwa na hali kama waliyonayo wapemba
si katika miaka ya mbali. Jee mko tayari yatokee hayao jamani?
Wazanzibari tulioko bara tunaambiwa tusijishughulishe na Siasa wakati
wenzetu wa bara wanapokuja zanzibar hukaa miaka miwili tu na mwaka wa tatu
akaanza kugombania uongozi na bahati mbaya tulivyokuwa hatuna uzalendo
tunawapa uongozi na kuwaacha Waunguja na Wapemba.Jee baada ya miswada hiyo
ijayo na myengine kufuatia baadae mnafikiri ndugu zangu tutasalimika? Jee
wazanzibari tutakuwa na uwezo wa kusema kama Wazanzibari Bungeni?
Wazanzibari tafadhalini kuweni kitu kimoja katika Maslahi ya nchi yetu.
Ndugu zangu wabunge wa CCM na CUF tafadhalini linapokuja suala la maslahi ya
nchi yetu na vizazi vyetu basi tafadhalini Muungane, muwe kitu kimoja
kuitetea sehemu yetu ya Muungano na isiwe sisi kugawiwa na kuwa dhaifu
katika Maamuzi muhimu yanayohusu nchi yetu.
Inasikitisha sana kuwa imefika Mzanzibari kusimama mahakamani na kueleza
kuwa zanzibar si nchi.na Rasia ni wa nne
kimadaraka.Tunagombanishwa na kutawaliwa.Kwa nini Upinzani ukae bara,
salama,na wakati huo huo serikali ya Muungano iwe inajigamba kuwa CCM wa
zanzibar ni wenzao? Bali upinzani upate nguvu kidogo na uweze kuisumbuwa
serikali ya zanzibar ili wawe frustrated na miswada ifanywe na bila ya shaka
kwa usalama wao hawatoweza kukataa. Tafadhalini tujifunze katika miswada
iliyopita ni matokeo yake? Wabunge wetu wa CCM mkishaipitisha miswaada hiyo
ya huko Bungeni ambayo pengine baadhi yake ni madhara kwa zanzibar
msifikirie, hata kama mmekubaliana,kuwa Serikali ya Muungano itawakubalia
kufanya mtakavyo Zanzibar pindi wao wakihisi hakuna maslahi kwao. Ng'o.
kwa hiyo tusiwape nguvu zetu wakazitumia na wakati tutapotaka msaada wao
wakatugeukia.
Jamani Wabunge wa wazanzibari (CCM na CUF) tafadhalini msigawike katika
kuyateteya maslahi yetu bungeni kwa Muungano. Ikiwa haya ninayosema
hamyaamini, tafadhalini tizameni mifano ya Yugoslavia na Kosovo, Yugoslavia
na Bosnia, Tizameni sababu za Waislam kupinduliwa na kuuliwa na kufukuzwa na
kupigwa marufuku Uislam Spain. Jee Wazanzibari mko tayari muambiwe au
kumrishwa kuwa Adhana ni marufuku kusomwa kwa kipaza sauti? Ikiwa
tutaendelea kugombana wenyewe kwa wenyewe hayo hayako mbali ndugu zangu.
Ndugu zangu wabunge,maisha yenu hapa ardhini ni mafupi sana na maisha ya
baadae akhera ni marefu sana. Tafadhalini msisahau akhera zenu kwa kwa ajili
ya ushindani wa kuwa lazima nikushinde na bora litote lakini nyinyi
msikaribie utawala. hao mnaogombana nao ni wazanzibari wenzenu, waisalamu
wenzenu na after all ni jamaa na ndugu zenu. Jee bora aje kutawala mtu wa
mbali zanzibar kuliko kutawala Mmatemwe, au Mmakunduchi au Mmicheweni, au
Mkengeja jamani? Tafadhalini tunakuombeni sisi watoto wenu mtizame
tunakokwenda tusiharibikiwe jamani.Kama ni makosa yaliotokea mpaka Rais wetu
akawa hana madaraka katika Muungano, basi jamani tafadhalini tusiyarudie.
Itafika wakati nyinyi wabunge wetu leo mtakuwa wazee na sisi watoto ndio
vijana na tutataka kuongoza nchi yetu kulingana na jamii yetu bali kwa
sheria mnazozipitisha nyinyi leo tutashindwa kufanya hivyo na mfano wa
karibu sana ni masuala ya zanzibar kujiunga na OIC,na zanzibar kuwa Custom
duties na taxes wanazohisi zina maslahi kwao. Jee tumeweza?
Yako mambo mengi sana yatakuja zaidi na zaidi ikiwa hatutokuwa waangalifu
tukashirikiana katika Mambo yanayoihusu Zanzibar. Ikiwa wewe Mbunge
mwakilishi wa watu Wa Zanzibar Bungeni utajali Maslahi binafsi au ya chama
chako tu bila kujali Zanzibar kama nchi au sehemu ya Muungano, nani
atayatetea maslahi ya Wazanzibari huko.
Jamani takriban nyote muliochaguliwa Ubunge ni wasomi au watu wenye uzoefu
katika siasa, tafadhalini msifanye mchezo na nchi yetu. Chama ni chama
lakini nchi si chama. Na nyinyi kumbukeni nyote ni wananchi Wazanzibar.Hata
kama utakwenda Uganda ambako pia ni Afrika utaitwa mzanzibari,ukenda kenya
ni hayo hayo, ukinda kukaa mwanza ni hayo hayo hata kama una asili ya
kisukuma na hutopata haki na hadhi kama watayopata wenyekuzaliwa pale.
Jamani tusijidanganye, tunaumia. Jamani thamani ya nchi yako huwezi
kuilinganisha na kitu chochote.Ndio utu wetu, ndio starehe, ndio uhuru, nk.
Tizameni watu kama Wapalestina walivyohangaika na mpaka leo wanapata tabu.
popote walipo hawana raha na kwao hakurudiki.Na wanakutaka lakini wapi,
wanakusikia tu wengine.Na wengine pamoja na raha walizokuwa nazo katika nchi
mbali mbali ilipopatikana fura ya kurudi walirudi. Si Wapalestina tu, bali
hata Waezraeli yaliwakuta majambo na miqasa ya nchi.Jamani mtu kwao.
Jee Wazanzibari hamjuwi kuwa "Mtu Kwao"? eeennnn!!!
Kwaherini na ahsanteni sana kwa kuisoma risala hii refu lakini naamini
umefaidika. Nakuombeni ndugu zetu mliokaribu na walioko madarakani hivi sasa
muwafikishie jamaa zetu ujumbe huu na ishaallah mema hauozi katu.
Atayefanya wema anaifanyia nafsi yake (ni wake huo), na ataefanya ubaya
ajuwe kuwa uko shingoni mwake na atakutana nao duniani au mbele ya haki au
mwote muili. Tunamuomba Mola wetu atujaaliye tuwe katika watu wanaosikiliza
maelekezo mazuri na wakayafuata.
Ndugu yenu.
Abdul.