Author :
Dr M Hassan
Date:
Sun, 16 Jan'00
Subject:
KATIBA YA ZANZIBAR
Ndugu wanamember,
Napenda kumuunga mkono ndugu forouk kwa maelezo yake juu ya matengenezo au
ubadilishanaji wa katiba ya Zanzibar,
kwa kweli hili ni suala linalowahusu wazanzibari wote awe ndani ya nchi au
nje ya nchi litatuhusu sote,lakini sasa vimewekwa vyombo maalum vya kujadili
mambo haya ya katiba kama baraza la wawakilishi la zanzibar ambalo ndilo
lenye mamlaka makuu ya kubadilisha katiba ya zanzibar,
masuala ya kujiuliza sisi wenyewe kabla ya kuingia kwenye huo mkondo wa
mageuzi ya katiba kwa ufupi ni kwamba,
1.Ni nini azma namadhumuni ya ubadilishaji wa katiba?
2.ni faida gani tutakayopata sisi wazanzibar juu ya hatua hiyo.
3.Hivi ni wakati muafaka kweli umefika wa kufanya mabadiliko hayo ya katiba
ili kuwendana na wakati au ulimwengu wa sasa.
4.jee wananchi wameelimishwa faida na hasara ya mageuzi hayo isijekuwa baada
ya mageuzi tunapata wafalme tele au marais wa maisha kwetu huko zanzibar na
wananchi sijui watamlaumu nani.
Baada ya masuala hayo machache napenda kuwaomba wale wote watakaobahatika
kuwepo kwenye hayo mageuzi ya katiba kutumia nafasi hiyo kujadiliana vizuri
na kutekeleza matakwa ya wananchi waliowengi sio kuangalia matakwa ya
kikundi au chama fulani cha siasa,mambo hayawi hivyo siasa za kijomba
zimeisha sasa ni kazi moja tuu kuleta maendeleo ya nchi yetu,tunadharaulika
duniani kwa sababuya umaskini unaotunuka daima,na hii si dunia ya kuhadaana
tena ni kujikaza kuleta maendeleo ya nchi katika nyanja zote za uchumi,na
jamii,
tusikimbilie kwenye mabadiliko ya katiba tuu ndugu zangu,tung'ang'anie
maendeleo pia,nchi inahitaji wataalamu na wasomi ili iendelee,na sote
tukimaliza kusoma huku nje tunabanisha kimya ulaya haturudi,sio kama watu
hawataki kurudi lakini mazingira yetu zanzibar sio ya kisomi,usome usisome
sawasawa na yule aliemaliza darasa la 11 haileselasie,sisi hatupendi kukaa
huku nje zanziabr yetu ni nzuri tuu,lakini tunajiuliza tukirudi tuna nini na
nani wa kutuelekeza jinsi ya kuanzia at least hiyo kazi japo ya kupiga soga
offisini.
Kwa kweli zanzibar bado tuna kazi kubwa sana sio hiyo ya mageuzi ya katiba
tuu,maendeleo na maendeleo bila ya ushirikiano wa pamoja ni ndoto tena ya
alinacha.na zanzibar kasoro yetu kubwa ni umoja na ushirikiano hatuna hayo
naona ni kilema chetu cha siku nyingi na hakiwezi kuondoka daima.
Al-muhimu nawatakia kila la heri na mafanikio huko nyumbani zanzibar mufanye
mabadiliko hayo ya katiba kwa usalaama na amani kusiwe na uvunjaji wa amani
wengine tuna vizee vyetu huko au twambieni tuje tuvichukue na wao waje kula
matunda ya mama ulaya.
ahsanteni
drhassan
London.
>From: Farouk Abdulla Amour
>To: zanzinet
>Subject: [zanzinet] MATENGENEZO YA KATIBA YA ZANZIBAR
>Date: Sun, 16 Jan 2000 22:31:43 GST
>
>Nduguzangu,
>
>Assalaam Alaaykum,
>
>
>Kwa muda yalianza kutajwa ya kwamba Dr. Salmin anataka kubadilisha katiba
>ili aweze kusimamia uraisi kwa mara ya tatu. Upande wa pili ilikuwa
>inatajwa ya kwamba hili linapingwa. Bara ilikuwa haikuthibitisha msimamo
>wake katika suala hili. Sasa ghafla imejitokeza ya kwamba inafanya kamati
>kushughulikia suala hili. Hivi maana yake ni kwamba Bara na wao watakuwa
>na
>mkono wao kamili katika suala hili, sio ajabu wakawa wao ndio wenye mkono
>wa
>juu zaidi kuliko Zanzibar ambao ndio wenye kukhusika khasa na suala hili.
>Huu ndio uhodari wa kisiasa. Usijiweke nje, kuwa ndani; na ikiyumkinika
>chukua sehemu kubwa na muhimu katika kila suala. Jamaa ni mabingwa wa
>siasa.
>Ikiwa huu ndio ubingwa wa siasa, jee kugomea kushiriki katika suala hili
>inazingatiwa ni nini katika siasa?
>
>Kutokana na hali hii, nina penda kuomba kwa kuwambia wa nje ya kwamba:
>"Ondoweni mikono yenu juu ya Zanzibar", yaani iwachilieni Zanzibar apange
>na iamue katika mambo yake wenyewe bila ya kuingiliwa. Zanzibar tunao uwezo
>wa kimaarifa na ujuzi wa kutosha, iwapo tutahitajia msaada tutakuarifuni,
>lakini tafadhalini tuachilieni musituingilie katika mambo yetu. Sisi na
>nyie ni ndugu, tunakaribisha kushirikiana lakini tunakataa kuingiliana.
>Muhimu zaidi ninaomba tuache mtindo wa kugomea, kugomea sio siasa;
>kushirikiana na kujadiliana ndio siasa. Madhali lipo Baraza ni wajibu wetu
>tulitumie Baraza mwisho wa uwezo wetu katika kueleza maoni yetu. Ninaomba
>Wawakilishi watekeleze wajibu wao wa kuwawakilishi wananchi katika kila
>mambo ya nchi yao, khasa katika mambo muhimu kama haya. Tunaomba Baraza la
>Wawakilishi kwa kushirikiana bega kwa bega walishughulikie hili suala la
>matengenezo ya katiba kwa maslaha ya Zanzibar, wala sio kwa maslaha ya mtu
>binafsi, kikundi cha watu au chama, makusudio iwe ni kutengeneza kwa faida
>ya Zanzibar, vizazi vyetu na jamii ya binadamu.
>
>Kwa kumaliza ninawaomba nduguzangu katika ukumbi huu tutoe rai na
>mapendekezo yetu katika matengenezo ya katiba ya nchi yetu. Ni wajibu wetu
>tutoe maoni yetu, na Inshallah wanaokhusika watayazingatia na kama
>itakavyofaa Inshallah yatasaidia.
>
>Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu azidi kutusaidia tuweze kujisaidia katika
>hili na kila la kheri na kutuepusha na kila la shari - Amin.
>
>Wa Billah Tawfiq
>
>
>Farouk
>
>