Author : Hashil Seif Hashil
    Date: Mon, 17 Jan'00
Subject: WACHENI KUBWABWAJA UKABILINI UKWELI ULIVYO

From: Hassan O. Ali
Subject: "WACHENI KUBWABWAJA UKABILINI UKWELI ULIVYO" (fwd)


---------- Forwarded message ----------
Date: Mon, 17 Jan 2000 11:19:10 +100
From: Hashil Seif Hashil 
To: hassan
Subject: "WACHENI KUBWABWAJA UKABILINI UKWELI ULIVYO"

Dear Hassan O. Ali,                                            17.01.2000


Natumai nyote huko muliko mwabesa na kuendelea na harakati za 
kimaisha za kila siku. Na sisi ndugu zenu tulioko ngambo ya pili 
wazima kama chuma cha pua.


Kama ujuavyo kinapotokea chochote kile cha kutukoroga vichwa 
vyetu; moyo wetu unakuwa hautupi kukaa kimya bila ya kutowa 
mchango wetu japo mstari mmoja. 

Kwa hivyo ningekuomba niliyonayo moyoni warushie Wazanzibari 
wenzangu waoni dukuduku langu:


            " WACHENI KUBWABWAJA UKABILINI UKWELI"


Nimejaribu kwa upande wangu kufatiliza huu mjadala uliopo hivi 
karibuni uliochokorwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa 
Serikali ya Muungano Hakimu Joseph Sinde Warioba kuweza 
kuikwaruza kovu kwa msumari, wakati alipotamka:" kuendelea 
Dk.Salmin na wadhifa wake kwa awamu ya tatu kuwa ni kuleta 
Usultani".

Msemaji wa Serikali ya (SMZ) Bw. Hafidh Ally amekuja juu mithili 
ya mtu aliyetia moto kwenye pango na ndani yake alikueko nyoka 
amejipumzisha wakati amesha mmeza mbuzi mzima !

Hakimu Joseph Sinde Warioba "kawatukana kistaarabu"; lakini 
hawakumfahamu hata kidogo. Ole wao. Hivyo kweli Warioba hajuwi 
maana ya Usultani ?. 

Kwanza yeye inafaa ifahamike kuwa ni Mwanasharia na kaliangalia 
jambo linalotaka kufanywa na Serikali ya Zanzibar huenda likaleta   
hatari kwao na vile vile kwa Muungano wa nchi mbili yaani 
Tanganyika na zanzibar.

Kubadilisha KATIBA siyo jambo la masihara hata kidogo.Kwani 
katiba ni kama "uti" wa mgongo kwa mwanaadamu.Haiwezekani 
hata kidogo watu kufanya utani na katiba ya nchi bila ya ridhaa ya 
wananchi wote waishio kwenye visiwa hivyo.

Ukiwasikiliza kwa makini sababu zao za kutaka kuibadiliska katiba 
katu haziingii akilini hata mtu akijaribu kuvuta Bangi. 

Wanavyojigamba kuwa Umma wa Visiwani wanamtaka Dk. Salmin 
Amour aendelee kuwa Rais wa nchi hiyo kwa sabab ya Kiuchumi 
na Siasa. 

" Ninani unafikiri atakaye weza kununua bidhaa hiyo 
wanayoitangaza". Na akina nani hao wanaowasemea kuwa 
wanamtka Dk.Salmin aendelee !!!!!!!!!  

Suala liliopo hapa ni kama ifatavyo: Kwanza hawa ndugu zetu 
wanaopiga makelele kama  kumfanyia 
kampeni Dk. Salmin Amour aendelee kutawala watufahamishe vitu 
viwili kwanza. Kwani lazima ziko < skuli mbili > za kulimungunya 
suala hili:

(a) Kama Dk. salmin Amour kawapa "taa ya kijani" (green Light) 
wamfanyie hii kampeni wanayoifanya ya kutaka kubadilisha katiba 
ili imfanye asimamie tena Urais kwa awamu ya tatu.

(b) Au wanayoyafanya ni kwa ajili ya kumfurahisha ili matakwa yao 
yakifanikiwa Dk.Salmin Amour aweze kuwapandisha vyeo na 
kuwapa marupurupu kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Vile vile, ikiwa kweli wanampenda Dk. Salmin Amour kwanza 
lazima wawafahamishe wananchi sababu za kutaka aendelee 
kwenye awamu ya tatu kwa sababu zifatazo:

(1) Kuwa toka Dr. Salmin alipoanza kuwa Rais wa visiwa hivyo 
ameweza kunyanyua hali za wananchi kwa fani mbali mbali.

(2) kuwa Elimu kwa watoto wetu imekuwa bora kuliko hapo kabla

(3) Kuwa hospitali madawa yamejaa na magonjwa mbali mbali 
ambayo yaliyokuwa hayawezi kutibika hapo kabla kwa upungufu 
wa Madaktri sasa yametoweka.

(4) Kuwa watu hawakamatwi ovyo-ovyo na mtu yeyote yule 
anayekamatwa lazima apelekwe mahakamani yafikapo masaa 24.

(5) Kuwa uhalifu wa kuvunjiwa watu majumba na kuporwa vitu vyao 
umeshaanza kufifia..

(6) Kuwa wanafunzi wakimaliza skuli makazi yanawangojea.

(6) Kuwa vijana wengi wanabakia nchini badala ya kwenda nchi za 
nje kutafuta kazi kwa sababu mahitajiyo yao yameshasawazishwa. 

(7) Uhalifi umepunguwa kwa sababu wananchi wanaridhika na hali 
ya kimaisha ya kila siku hapo nchini.

Hayo ni machache tu niliyoyaeleza ili iwe kama "chambo" cha 
kuwawezesha wananchi kuona kweli Dk. Salmin Amour anastahiki 
kuendelea kwa awamu ya tatu pindipo katiba ikibadilishwa kwa 
kazi nzuri aliyoifanya.

Pia nimeona nigusie kitu ambacho sifikiri kama kinafaa kuendelea 
na jina aliloliacha hayati Mzee Abeid Amani Karume: "Kuwa jela ni  
pahala pa chuo cha mafunzo". 

Nafikiri wakati umefika kuweza kuita jela kuwa jela siyo chuo cha 
mafunzo.

Kwanini nikasema hivyo: Hakuna kati yetu asiyejua mambo 
yaliyokuwa yakitokea kwenye hivyo wanavyoviita "vyuo vya 
mafunzo", wananchi kutolewa usiku kwenye vyumba vyao na 
kwenda kuteswa na kuuwawa. 

Wakati wanaoendesha serikali bila hata kuona haya na vibaya 
kuendelea kuita sehemu hizo kuwa ni "vyuo vya mafunzo".

Nafikiri itakuwa uzuri kuvita vyuo hivyo sehemu za . 

Kwani hakuna asiyejua ndugu zetu 18 mpaka leo wanaendelea 
kuteswa kiakili ndani ya hivyo wanavyoviita:" vyuo vya mafunzo". 

Hebu tuelezeni kinaga-ubaga hayo masomo munayowapa hao 
ndugu zetu 18 toka siku waliokamatwa mpaka hivi leo. Bila ya 
shaka watatoka na mashahada ya Phd, BA,nk, nk, nk........

Lazima ndugu zetu munaoendelea kuwatesa,siku yeyote ile 
mutakayo amuwa kutaka kuwatowa lazima kwanza muwatake 
radhi kwa kitendo mulichowafanyia cha kuwatenga na familia zao 
na vile vile muwape fidia kwa muda muliowaweka kwenye hivyo 
munavyoviita "vyuo vya mafunzo".

Wakatabahu

Hashil S. Hashil