Author :
Harith Ghassany
Date:
Thu 13 Apr 2000
Subject:
HISTORIA YA MZEE KARUME?
Assalam Alaykum Sheikh Khatib,
Suala la historia ya marehemu Mzee Karume limezongwa na masuala kemkem
ambayo bado yanangojea jawabu za utafiti na ushahidi wenye kuaminika.
Hivi karibuni Sheikh Issa Nasser Al-Ismaily katika kitabu chake cha
"ZANZIBAR: KINYANG'ANYIRO NA UTUMWA" kaandika:
"wakati mmoja, katika mkutano wake wa hadhara, Karume alijidai kwamba
utotoni kwake alisoma katika skuli ya Mwera. Kwa vile mimi nilisoma katika
skuli hiyo, nilikuwa na hamu kubwa sana ya kujua ukweli huo. Nilikwenda
skuli ya Mwera katika mwaka 1961 na niliyapitia madaftari yote ya majina ya
wanafunzi wa skuli hiyo tangu mwanafunzi wa mwanzo mpaka pale lilipoanzia
jina langu mimi katika mwaka 1938, lakini kabisa sikukutia jina la Karume"
pp. 120-121.
Mwenye kusoma maneno ya hapo juu ataweza sana kufikia kuamini ya kuwa Karume
alisema uongo na mwaandishi katoa ushahidi wa kukanusha maneno ya anaedai
kuwa alisoma skuli ya Mwera.
Suala liliopo hapa ni skuli ipi ya Mwera aliyosema Karume kasoma? Ndio hiyo
aliosoma Sheikh Issa Nassor au pana skuli nyengine Mwera ambayo mwandishi
haijui?
Skuli aliosoma Karume sio kabisa hiyo aliosoma Sheikh Issa 1938. Skuli
aliosoma Karume ni pale penye kijisikiti kidogo Mwera Police Station kiliopo
mkono wa kushoto. Ikiwa unakwenda Dunga au Koani ipo sehemu ndogo sana ya
huo msikiti ambapo siku panawekwa jeneza. Hapo ndipo aliposoma Karume hata
kabla ya kujengwa skuli ya Mwera anayoizungumzia Sheikh Issa Nassor.
Katika wazee waliosoma na Karume ambao wahai ni Sheikh Issa Al-Shammakh
ambae anaishi Kiembe Samaki, Unguja. Marehemu Mzee Juji wa Mwera alikuwa na
kumbukumbu kubwa ya historia ya Mzee Karume.
Kuhusu wapi kazaliwa na lini, inavyosemekana ni kuwa Karume alikuja Unguja
mtoto wa mgongoni na mama yake alikataa kutoa ushahidi kortini pale
alipotakiwa kutoa ushahidi kama mwanawe kazaliwa Unguja au la.
Pia kuna maneno ya kuwa Sheikh Rashid bin Slim Al-Gheithy na Sheikh Said bin
Abdalla Al-Kharusy ndio waliomdhamini Karume kuwa kazaliwa Zanzibar ili
atolewe pasapoti ya kusafiria. Inasemekana pia kuwa birth certificate ya
Karume imeandikwa kuwa ni "Myasa" lakini kumbukumbu nyengine zinasema ya
kuwa alitokea Congo au alikuwa Mhutu kutoka Ruanda lakini alijiandika Myasa
kwa sababu Nyasaland ilikuwa ikitawaliwa na Waengereza basi kwa hivyo ikawa
ni rahisi kwake kukubalika Zanzibar shauri ilikuwa ikitawaliwa na hao hao
Waengereza.
Hizo zote ni hadithi ambazo zinangojea kuthibitishwa au kukanushwa.
Suala lipo pale pale: nini historia ya uhakika ya marehemu Mzee Karume?
Harith Ghassany.
>From: "Khatib Rajab"
>To: allysaleh
>CC: Zanzinet
>Subject: [zanzinet] Re: Ongozeko la wa Tanganyika
>Date: Wed, 12 Apr 2000 12:10:43 PDT
>
>Sheikh Ally
>Assalam alaykum:
>
>Ahsante sana kunisawazishia songombingo ya uzalendo wa Karume. Kwa kweli
>hata na mimi hiyo taarekhe aliyokuja Zanzibar sina uhakika nayo kwani
>nilipata kwa sauti ya mdomo.
>
>Pengine tarekhe aliyokuja na pahala alikozaliwa zinaweza kupatikana kwenye
>nyaraka za Zanzibar kama hazikuibiwa wakati wa utawala wake.
>
>
>Wassalam
>
>
>Khatib Rajab al-ZINJIBARI
>======================================================================
>>From: "Ally Saleh"
>>To: Khatib Rajab
>>CC: alinassor, Zanzinet
>>Subject: Re: [zanzinet] Re: Ongozeko la wa Tanganyika
>>Date: Wed, 12 Apr 2000 20:09:32 +0300
>>
>>Salaam,
>
>>Sijui, lakini hii ya 1938 nashindwa kuaamini.
>
>>inawezekana karume kazaliwa malawi lakini ni lazima ikiwa hivyo basi
>>alikuja mdogo sana.
>
>>kumekuwa na ushahidi kadhaa kuwa amekulia zanzibar.
>
>>ni hiyo ya 1938 haiwezi kuwa na ukweli kwa vile tayari katika miaka >ya
>>labda miaka ya 1916-1925 alikuwa baharia na walikuwepo watu >waliofanya
>>nae
>>kazi.
>
>>pia katika miaka ya 20 basi kulikuwa na juhudi za kuunda african
>>association basi nae pia alikuwa mbele. kuna ushahidi wa watu >waliofanya
>>kazi nae.
>
>>kwa hivyo kuja kwake 1938 hakuna ukweli.
>
>>ally saleh