Zanzibar
Organization
BISMILLAAHI RRAHMAANI RRAHIIM
"Na
shikamaneni kwa Kamba (Dini) ya Mwenyezi Mungu nyote
pamoja,
wala msifarikiane".
Wazee wetu, Ndugu zetu,
Assalaam
Alaaykum, UMOJA NA UHURU
SIKU ADHIMU KWA WAZANZIBARI
Kwa
Wazanzibari Disemba 10 ni siku adhimu katika taarikh ya nchi yao,
ni
siku inayoishi katika nyoyo zao kwa fakhari na machungu.
Disemba 10 inaishi
kwa fakhari nyoyoni mwa Wazanzibari kwa
kuwa ndio siku ya Uhuru wa nchi yao.
Siku ambayo Wazanzibari
waliirejeshea nchi yao - Zanzibar - Uhuru wake baada
ya
juhudi zao mbali mbali na kwa kujitolea kwa hali na mali. Disemba
10
inaishi katika nyoyo za Wazanzibari kwa machungu na huzni
kwa vile Uhuru wa
Zanzibar na Zanzibar huru haikuishi zaidi
ya siku thalathini na tatu, bali
ilivamiwa na kumezwa na
Dodoma chini ya kisingizio cha muungano. Huo ukawa
ndio
mwisho wa Zanzibar na mwanzo wa masaaibu yote ya Zanzibar. Kwa
munasaba
huu adhimu, yaani leo kufika miaka 37 tangu ile Disemba
10, 1963;
tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na tunawaombea dua
wazee wetu na ndugu
zetu waliotangulia mbele ya Haki na waliopo
ulimwenguni kwa juhudi zao hizo,
Mwenyezi Mungu awajazi kila la
kheri duniani na Akhera - Amin. Dua zetu
vilevile
ziwafikie wazee na ndugu zetu waliouliwa mashahidi katika ghasia
za
Juni 1961 na katika mavamizi ya Januari, 1964 na mashahidi
wetu wote wengine
wa kabla na wa baada – Mwenyezi
Mungu awarehemu na awatie Peponi kwa Rehema
Zake –
Amin. Kwa munasaba huu, munasaba wa furaha ya wiki chache
na
munasaba wa msiba na masaaibu yanaoendelea mpaka hii leo,
Umoja wa
Wazanzibari – Zanzibar Organization -
kwa hishima unaleta mbele yenu humu
barazani haya yafuatayo
ili tushirikiane katika kuzingatia na tufikiri kwa
pamoja namna
ya kutengeneza kwa maslaha ya Zanzibar ya leo na ya kesho.
DOLA
HURU YA ZANZIBAR
Kwa Rehma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na juhudi
za Wazalendo wa Kizanzibari
wazee wetu katika uwongozi
wa “Umoja wa Wazanzibari” (ZNP/ZPPP), manamo
saa
sita na dakika moja za usiku wa kuamkia taarikhi 10 Disemba
1963;
waliirejeshea Zanzibar Uhuru wake na kuwa ni Dola Huru
Kaamili miongoni mwa
dola za ulimwengu. Katika kutekeleza
jambo adhimu hilo, bendera nyekundu
iliteremsh-wa kutoka
kwenye mlingoti wake na Bendera ya Dola Huru ya
Zanzibar
yenye karafuu mbili (zikimaanisha visiwa viwili vya
karafuu, Unguja
na Pemba) ilipandishwa na kupepea
katika mlingoti uliokuwepo kwenye ardhi ya
Zanzibar
katika uwanja wa Mivinjeni (Coopers Insititute). Kwa vile
Zanzibar
haikuwa koloni ya Muingereza, basi haikuwepo bendera
ya Kiingereza
kuteremshwa, kwa sababu haikupatapo kupepea juu
ya ardhi ya Zanzibar.
Japokuwa Zanzibar ilitiwa kwa mbinu za
Waingereza chini ya himaya ya
Kiingereza, haikuwa koloni kama
vile koloni nyenginezo za Kiingereza.
Zanzibar haikusita
kuwa Dola kwa muda wote iliokuwa chini ya himaya ya
Muingereza,
iliendelea kuwa Dola na kila lake na chake. Zanzibar
imesita
kuwa Dola baada ya kuvamiwa na kutiwa chini ya makucha
ya Dodoma pale 1964.
SHEREHE ZA UHURU
Wananchi wote wakubwa
na wadogo, wanaume na wanawake, waliupokea Uhuru wa
nchi
yao kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa furaha
na bashasha
kubwa. Mji ulikuwa ukin'gara kwa mapambo ya
namna mbali mbali. Tamasha hizi
na zile zilifanywa na wananchi
kwa kufurahikia Uhuru wao. Sherehe na mapambo
hayakuwa Mjini tu,
bali mashamba kote. Na huko Pemba nako kulifanywa sherehe
kama
za Unguja, tangu mijini mpaka mashamba. Wazanzibari walijaa tamaa
na
matumainio ya kwamba baada ya juhudi na kazi ngumu ya
kuleta Uhuru wao na
kwa kuondoka mtawala Muingereza sasa
wataweza kushirikiana Wazanzibari wote
bila ya ubaguzi wa
aina yoyote ile katika kazi ngumu na ndefu ya kujenga
nchi
yao kwa masalah ya nchi yao. Tamaa na matumainio haya yalitokana
na
imani yao Wazanzibari juu ya uwongozi wa umoja
wao - “Umoja wa Wazanzibari”
-
uliojengeka katika misingi ya uadilifu wa haki sawa kwa wote.
Haya, yaani
uadilifu wa haki sawa kwa wote yalithibitishwa kwa
vitendo kama vile
alivyotueleza Sheikha Ali Muhsin katika kitabu
chake: “Conflicts and Harmony
in Zanzibar”,
yeye katueleza haya yafuatayo:
ZNP/ZPPP FOR ALL PEOPLE.
Our
very restricted resources compelled us to have our diplomatic offices
in
New York also accredited to Washington, in London accredited
to the rest of
Europe, in Cairo to cover the rest of the Arab
world, and in due course
Indonesia, which was importing the
greatest share of our clove production,
to be the base for
the rest of Asia.
While we made certain that the ambassador and
the counsellor (his second in
command) were our political
nominees, being supporters of the ZNP/ZPPP
alliance, we appointed
the first secretaries by virtue of merit irrespective
of
their political affiliation. Thus the first secretary to the UN
embassy
happened to be Khamis Hassan Ameir, to the Cairo
embassy was Ali Khamis
(once speaker to the Zanzibar House of
Representatives), and the would-be
first secretary to Indonesia
was to be Ali Hassan Mwinyi. (he later became
President
of Tanzania.) All three were known to us as supporters of
the
ASP. Professionally they had the capacity to fill the
posts, and that was
all that mattered to us. It was not very
easy to convince everybody in our
party's national executive
of the fairness and wisdom of making these
appointments, but I
did manage at last to get unanimous support by reminding
my
colleagues that ours was, from the very beginning, a vanguard
party
working for the whole nation and not for a segment
of the population.
Such and other measures began to have a
telling effect on the more thinking
section of the opposition,
particularly the younger educated elements
aspiring for higher
things in the future. They were pleasantly surprised to
find
that the ZNP/ZPPP government was being fair and just, and that
it
assessed people according to merit irrespective of their
political
connections. There was even some talk about their
joining the ruling
alliance en masse. This was a threat to the
semi-literate leadership of the
ASP, the newly created Umma
party and their common boss across the channel.
The longer the
government stayed in power the more popular it was bound to
make
itself, and the more likely the opposition would be losing
support.
Thus was it imperative that the rebellion had to take
place as soon as
possible. And thus it was that after the general
massacre of the thousands
of the ZNP/ZPPP supporters Karume and
his immediate thug supporters began
murdering one by one the
educated elements in the ASP whom they had always
suspected
of considering changing their allegiance. Othman Sharif,
Kasim
Hanga, Mdungi Usi, Twala, Jaha Ubwa and many others were
liquidated. Dr.
Kingwaba was disgraced. From being a successful
qualified medical officer he
was put in charge of the post
office. Dr. Ahmed Rashid, a veterinary
officer made into
a Director of Economy, had to flee for his life. He died
in
Britain.
(Conflicts and Harmony in Zanzibar – page
216)
“Umoja Wa Wazanzibari” katika misingi yake kuwa
ni Umoja wa Wazanzibari wote
ulitekeleza mipango yake yote
katika misingi hio. Wazanzibari walitambua
vyema kuwa baada ya
hivi kupatikana Uhuru kulikuwa na kazi kuu mbele yao,
yaani
kujenga nchi ni kazi ndefu na ngumu sawa au zaidi kuliko ile ya
kuleta
Uhuru. Juu ya hivyo, walikuwa tayari kubeba
jukumu hilo kwa azma na shajaa
kwa sababu imani yao ni kwamba
utumishi wa nchi ni wajibu wa kila mwananchi
na ni wenye
kuhisabiwa na kulipwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
ZANZIBAR
INAJIUNGA NA UMOJA WA MATAIFA
Baada ya kupata Uhuru wake Zanzibar,
taarikh 14 Disemba, 1963 ilijiunga na
Jumuia ya Umoja wa
Mataifa (UNO) ikiwa ni mwanachama kamili wa Jumuiya hio
ya
kilimwengu. Kwa munasaba huu nina inukulu hapa (tena) khutuba
ya Waziri
Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Muhammad Shamte
katika Umoja wa Mataifa (UNO)
taarikhi 16 Desemba,
1964 ikikaribishwa Zanzibar kuwa ni mwanachama wa
Jumuia
hii muhimu ya kilimwengu.
A REMINDER SPEECH
Prime
Minister Muhammed Shamte Hamad (as Head of Government of
the
independent and Sovereign State of Zanzibar) delivered the
following
historic speech on the historic day of 16th December,
1963 to the General
Assembly of the United Nations Organization
in New York.
Mr. President!
It is a very great honour and a very
great pleasure for me to be here as
Zanzibar's representative
at the moment when Zanzibar's application to join
the
United Nations Organization has been accepted by the General
Assembly.
Zanzibar's entry to this great Organization is
to my mind of special
significance, and this is that there is
no country so small and so modest in
its means that it cannot
be represented here in equal terms with the great
nations
of the world. There are some people who consider this scheme
of
things to be wrong. But I consider it to be a source of
strength to this
Organization, and that one that will inspire
Zanzibar to use its privileges
with a sense of responsibility
and dedication to the ideals which prompted
the establishment of
the United Nations.
To our many friends throughout the world who
have done so much in supporting
our struggle towards national
liberation, to the Decolonization Committee
which has contributed
so much in speeding up our march to Independence, and
to this
august Organization of the United Nations to which we owe so much,
I
would like to convey my country's deep gratitude. To
them we continue to
look for aid and support in the upliftment
of our people so that we may also
be able to contribute our
humble share towards the solution of the world's
problems. To
the distinguished delegates in the Security Council and in
this
General Assembly who paid tributes to the struggle and
achievements of my
country I would like to convey the sincere
gratitude of my delegation. To
all those who have sponsored
our application, and to all the distinguished
delegates who have
unanimously voted us into membership of the United
Nations,
I say: Thank you.
Mr. President. Political problems tend
to hit the world headlines, but it
is not generally known,
for instance, that malaria which a few years ago
used
to cause as much havoc as any war, is now almost wiped out
from
Zanzibar, as a result of an intensive joint effort
on the part of WHO,
UNICIEF and the Government and people
of Zanzibar. It is also not known
that quietly but
determinantly we are trying with the aid of the ILO and FAO
to do
away with the curse of under-employment. There are many other ways
in
which individual countries and international organizations
have been
co-operating with us in solving our problems.
We are grateful to them all.
Now that the energies of our people
are unleashed by the restoration of our
national pride and
sovereignty we can look forward with confidence to
greater
and more comprehensive assistance from every quarter. Zanzibar
is
one of the smallest nations in terms of population and
size to be accepted
for membership. This in itself
entails sacrifices for Zanzibar, sacrifices
which are of little
significance to nations of great wealth, but are of very
great
concern to us of slender means. These sacrifices we are very glad
to
make. If we are not rich in numbers, in territory,
in material wealth we do
not count ourselves poor in values
of life which are so inestimably more
important; and it is
because of this that we feel we can contribute, even if
only
modestly, in the affairs of this Assembly.
We have a long
and honourable history and civilization behind us. Like
so
many of the great peoples of the world our roots are sprung
from many
different sources, from Africa primarily, but also from
Arabia, from the
civilization of Asia, Persia, from India and
from many others. The
Europeans in their great voyages of
exploration found succour and sustenance
on our shores. And
men of many races found rest and stability in our
islands from
where to organize the exploration and development of Central
and
Eastern Africa It is due to these roots established over centuries,
the
mixing of so many cultures, that make us proud of our
reputation for
moderation and friendliness. While
in the modern world we do not intend
looking back to our
past, it is this tradition on which we intend to build
our
future.
Zanzibar is a constitutional monarchy founded on liberal
and democratic
traditions, governed by a Prime Minister and a
Cabinet of elected Ministers,
with collective responsibility
and answerable to a National Assembly elected
on the basis
of universal adult suffrage. The Fundamental Human Rights
to
personal liberty and protection against discrimination are
entrenched in
Zanzibar's Constitution. Our overall aims
are peace and progress at home
and abroad. The chief
object must be to help create a political atmosphere
in
the world in which man's real enemies of hunger, ignorance and
disease
can receive full attention so that resources and
time are not wasted on
fruitless matters of dissension.
Zanzibar's general policy is one of
benevolent and positive
neutrality without discrimination against any
country
on grounds of race, creed, culture or ideology. It supports
all
measures of peace in the world on the basis of international
cooperation. On
the achievement of its independence Zanzibar
has freely elected to remain a
Member of the Commonwealth of
Nations, and it is fitting and pleasurable to
pay tribute to
the continuing harmonious relations which have obtained
between
Zanzibar and the United Kingdom. We believe in the Commonwealth
as
a large number of equal and sovereign states of many
peoples and cultures
who have voluntarily and democratically
joined together and are dedicated to
the furtherance of peace,
co-operation and prosperity throughout the world.
It is the object
of Zanzibar to strengthen the many ties it possesses with
both
Africa and the East. To this end we subscribe to the principles
of the
Bandung Declaration of 1955 and of the Charter of
the Organization of
African Unity framed at Addis Ababa this
year. Zanzibar has particularly
close relationship with
the other territories of East Africa, and it is our
intention
to continue this in friendship and co-operation, whether inside
or
out of a form of an East African Federation. In
this respect I am
particularly glad that Kenya with which
Zanzibar has so many close
connections is being welcomed
into this Assembly at the same time. At this
proud
moment in our history I may be permitted to quote Shakespeare and
say:
"We are two lions littered in one day."
Sir,
In submitting the application for membership for Zanzibar I have
made a
solemn declaration in common with that made by other
nations represented
here today that on behalf of my government
I have accepted the obligations
contained in the Charter of the
United Nations, and have undertaken to
fulfil them. This
solemn declaration is a very real one for me, and I pray
that
this indeed will be so, and that Zanzibar in future will honour it
to
the full. Thank you, Sir.
MAVAMIZI YA JANUARI
12, 1964
Ole wetu! vitumishi vilikuwa vimeshawekwa tayari na
mabwana zao kuufisidi
na kuuvuruga Uhuru, bali kuivuruga Nchi
na wananchi wake. Sherehe
hazikuwahi kumalizika, wala
majasho hayakuwahi kukauka mwilini kutokana na
juhudi na mbio za
kugombea Uhuru wetu, bali ghafla tulijishitukia katika
msiba,
tushavamiwa. Na huo ulikuwa ndio kuanzia kwa maafa ya Zanzibar
na
kupotea kwa kila kheri yake na kumezwa Dola ya Zanzibar
na kutiwa chini ya
makucha ya Dodoma kwa kisingizio cha
muungano.
Mafisadi wachache kwa ajili ya maslahi ya
nafsi zao hawakutahayari wala
hawakuona vibaya hata kidogo
kuchan-ganyika na wageni waliokuwepo ndani ya
nchi
na walioletwa kutoka nchi za jirani kwa makusudio khasa ya
kuivamia
Zanzibar na kuiondoa Serikali ya wanan-chi
na kuimeza Dola ya Zanzibar.
Wananchi mafisadi hao
walikubali kuongozwa na wageni, John Okello aliyetoka
kwao
Uganda, Injin aliyetoka kwao Kenya na Mfaranyaki aliyetoka
kwao
Tanganyika, kuivamia nchi yao katika siku wa
manane wa kuamkia taarikh 12
Januari 1964. Wananchi, mafisadi
kwa sababu ya maslahi ya nafsi zao
hawakuhisi uchungu wala
fedheha kuipoteza nchi yao, wala kuzipoteza roho za
wazee wao,
za ndugu zao na za marafiki zao. Kwa mujibu wa kitabu cha
huyo
aliyejipa ujamadari wa hayo 'mavamizi'
ya Januari 12, 1964, John Okello,
amesema kuwa watu
waliokufa (waliouliwa) katika 'mavamizi' hayo ni
13,000.
Hii ni idadi ndogo kabisa aliyopenda kuitaja
yeye.
Ukatili, ushenzi na unyama uliofanywa katika visiwa hivi
vilivyokuwa na
ustaarabu wa kupigiwa mfano, hauwezi hata
kuhadithika. Wengi waliokuwa
wanaijua Zanzibar, waliona
taabu kuyaamini waliyokuwa wameyasikia yametokea
Zanzibar
kutokana na hayo yenye kuitwa 'mapinduzi'. Ilifika
hadi, siku hiyo
ya 'mavamizi' majahil na makatili hao
ku-wanajisi maiti wa kike. Kitendo
hicho hakijapa-tapo
kufanyika katika nchi nyingi ulimwenguni zenye
ubinaadamu
na ustaarabu wake.
MWALIMU NA MAVAMIZI YA ZANZIBAR
Sote
tunakumbuka uzuri maneno ya Mwalimu aliposema, “Lau kuwa
nnaweza basi
ningali viburura Visiwa hivi (Zanzibar)
hadi katikati ya Bahari ya Hindi”.
Na hivyo ndivyo
alivyokuwa akifanya Nyerere mpaka kuondoka kwake ulimwenguni
na
ndivyo wanavyofanya warithi wake hadi hii leo, wamo kuviburura
Visiwa
vyetu kuelekea baharini. Tafauti iliyopo baina ya jana
na leo ni kuwa hii
leo vuta-ni-kuvute baina ya
Dodoma na Wazalendo wa Kizanzibari imezidi kuwa
kubwa kwa
vile kila siku upande wa wananchi unazidi Umma na
unazidi
nguvu. Umma unazidi kufahamu madhila ya kutawaliwa
na haja ya kurejesha
Dola yao Huru ya Zanzibar ili warejeshe
ubinadamu wao na waweze kuishi
kibinadamu.
KUMEZWA
DOLA YA ZANZIBAR
Sote tunafahamu ya kwamba mara baada ya mavamizi
ya Januari 1964, mwaka huo
huo; mwezi wa Aprili Zanzibar
ilitiwa chini ya makucha ya Dodoma kwa
kisingizio cha
muungano. Kutokana na “Articles of Unions” Zanzibar
ilipoteza
Dola yake na kuwa ni koloni la Tanganyika.
Mengi yamesemwa juu ya suala
hili, ya hivi karibuni ni
haya waliosema wao wenyewe, katika kitabu chake
“The
Political Plight of Zanzibar”, Profesa Maliyamkono katika
ukurasa wa
198-199 ametueleza haya kukhusu huu unaoitwa
muungano:
“Defining Union Matters
One of the thorniest
problems facing the Union has been that of deciding on
the
formula for the relative contribution of each part of the Union to
the
fiscal requirements of the Union. This requires first
a decision or what
government activities should constitute
Union matters. Constitutionally, the
Union matters have
their history in the “Articles of the Union”, signed
by
the two founders of the Union, Mwalimu Julius K. Nyerere,
on behalf of
Tanganyika, and Sheikh Abeid Karume, on behalf
of Zanzibar.
The Interim Constitution based on the Articles
of the Union, stated that the
issues for which the Union
Government and Union Parliament had direct
responsibility
were these:
1. The Constitutions and Government of the United
Republic
2. External Affairs
3. Defence
4. Emergency
Powers
5. Citizenship
6. Immigration
7. External Trade
and External Loans
8. The Public Service of the United
Republic
9. Income and Corporate Tax, Customs and Excise
Tax
10. Harbous, Civil Aviation Post, and telegraphs
It
is however, debatable whether all the above 10 areas are
exclusively
Union matters as the Interim Constitution may
have intended them to be.
Obvious queries arise with regard
to 7 & 8, for example. With regard to No.
7,
Zanzibar runs its own external trade and even keeps its own statistic
on
foreign trade and payments. As for No. 8 the implication
is that there is a
Union Service Commission.
There
is none.
The list of Union “matters” was
increased to 21 when the Constitution of the
United Republic
was published in 1997. These were:
11. All Banking and
Currency Matters
12. Industrial Licences and Statistics
13. Higher
Education
14. Petroleum Natural Resources
15. National
Examination Council
16. Air Transport and Communication
17.
Research
18. Meteorology
19. Statistics
20. United Republic
Court of Appeal
21. Registration of Political parties
Again
it is doubtful that all these additional activities are exclusively
on
effectively Union Matters
The Shellukindo
Committee (see below) expanded the scope of the Union
based
on the argument that most ministries in SMT have some
Union element. Thus
the Presidency is to a certain extent
a union matter. Every ministry in the
SMT which deals with
international agencies on behalf of the entire United
Republic is
involved in a “Union” activity. This is the widest
definition
of Union matters and the definition in the Interim
Government is the
narrowest.”
Ndugu zangu, huu ndio
muungano; muungano ambao tangu ulipoundwa ulikwisha
ipoteza
Dola ya Zanzibar kwa kunyang’anywa Zanzibar mambo 10 ambayo
ndio uti
wa mgongo wa Dola. Baadae polepole ndio 11
mengine kuongezwa na hapa
kuimaliza Zanzibar. Yote haya ni
kizungumkuti, hapana lenye kufahamika; ni
kuzongwazongwa
tu, lakini haya maneno: “Thus the Presidency is
to a certain
extent a union matter”, ndio zaidi
hayafahamiki. Jee Raisi wa Zanzibar ana
uwezo
gani? Kwa kumaliza muandishi ametwambia kuwa: “This is
the widest
definition of Union matters and the definition
in the Interim Government is
the narrowest”.
Kweli ilioje! Kweli ikidhihiri uwongo hujitenga.
Wazee wetu,
ndugu zetu, Wazanzibari huu ndio “muungano”
na hivi ndivyo
ilivyofikishwa Zanzibar ndani ya
huu “muungano”.
Matumainio yetu sote ni
kwamba sisi ni watu wazima na wenye fahamu kamili,
sio watoto
wadogo wala sio tusiofahamu. Mwenye macho haambiwi tizama.
Nini
la kutenda hili ndio suala muhimu, lakini la kutenda ni
lazima Wazanzibari
waamue na kwa haraka kwani kila tukichelewa
ndio khatari inazidi. “The
list
of Union “matters” was increased to
21 [when the Constitution of the
United Republic
was published] in 1977.” Hapa haioneshi kuwa
hii
constitution inayosemwa kuwa ilizungumzwa na kukubaliwa
na kila upande -
Zanzibar na Tanganyika -
kisha ndio ikawa “published”. Msiba ni
kwamba
inawezekana wakati wowote ule hii constitution
ikawa “published” na
kuongezwa orodha nyengine,
kama kiko bado ambacho hakijachukuliwa na kutiwa
ndani ya huyu
jini anaeitwa “Union matters”.
DHULMA NI MOTO
USIOKUWA NA BWANA
Kutokana na fisadi na fitina zilizokuwa zikiongozwa
na Nyerere na kusaidiwa
na mabwana zake pamoja na vibaraka vyao,
Zanzibar ilivamiwa na kutiwa chini
ya utawala wa Dodoma kwa
kisingizio cha muungano. Yote haya ni kuendeleza
vita
vya msalaba dhidi ya Waislamu. Walimwengu mbali mbali kwa
kusikiliza
fitina hizo - ambazo zilipandikizwa kuwa ati
iliopinduliwa Zanzibar ni
serikali ya Kisultani na Kiarabu -
walisherehekea maovu yote yale
yaliotendewa Zanzibar.
Wengi wa walimwengu walikuja Zanzibar kusherehekea
mauaji,
kunajisiwa binadamu – wake kwa waume, wakubwa kwa
wadogo;
kunyang’anywa watu haki zao, tujazwa magerezani
mamia ya binadamu bila ya
kosa na bila ya kupelekwa
mahakamani, kuwabidi mamia ya binadamu kuihama
nchi yao
bila ya kujuwa wanakimbilia wapi. Walimwengu walisherehekea
na
kuyakiri maovu hayo, walimwengu hao wakiwemo Waislamu walikiri
kutendewa
binadamu dhulma. Dhulma hii walifanyiwa Wazanzibari,
lakini walisahau kuwa
dhulma ni moto, moto hauna mipaka wala
hauna bwana. Moto huu wa dhulma
ulienea ghafla Afrika nzima,
kuanzia Afrika Mashariki na kwengineko.
Serikali kadhaa wa kadhaa
zilipinduliwa na watu kupata kila maafa, wengi
iliwabidi wazihame
nchi zao ili kukimbia maovu waliokuwa wakitendeana
wenyewe
kwa wenyewe. Mnyonge kudhiliwa ilikuwa ndio mtindo wa kila
siku.
Haya yote ni kwa sababu ilipotokea dhulma
Zanzibar hapana alieinua sauti
yake kuiteta, kinyume
chake, wengi waliikiri na kuisherehekea, kwa sababu
Nyerere
kawaambia kuwa waliofanyiwa hivyo ni kina sultani – kwahivyo
wanafaa
kudhulumiwa. Walisahau kuwa dhulma ni moto, hauna
mipaka wala hauna bwana.
HATUTENGENEKEWI MPAKA TUONDOE
DHULMA
Wazanzibari tusitaraji kupata Nusra ya Mwenyezi Mungu mpaka
kwanza tutake
toba ya kweli, hapo tena ndio tuombe Nusra ya
Mwenyezi Mungu ambayo ndio
pekee itakayo tuvua na maafa na balaa
hii tunayoishi nayo tangu pale
tulipoingia katika dhulma.
Toba ya kweli ina shuruti zake, miongoni mwa
shuruti hizo
ni kujuta kwa tuliotenda na kuazimia tusirejee tena kutenda
maovu
hayo. Vilevile shuruti zake ni kutenda mema kwa kuondoa dhulma
na
kuleta haki na kumpa kila mwenye haki yake haki yake.
Haiwezekani kujenga
haki na uadilifu juu ya dhulma, ni
lazima kwanza tuondoe dhulma ndio tuweze
kujenga haki na
uadilifu. Huwezi kupanda mmea ndani ya biwi la moto.
TUME
YA KUCHUNGUA DHULMA
Kwa makusudio ya kutengeneza na kutafuta Nusra ya
Mwenyezi Mungu kwa kuondoa
dhulma na kujenga haki na uadilifu
tunamuomba Bwana Aman ateue tume maalumu
ichungue juu ya dhulma
zote tulizotendeana na kupangwa njia ya kuziondoa
dhulma
hizo na kujenga haki na uadilifu badala yake. Kitendo hichi
ni cha
dharura ili tuweze kupata Nusra ya Mwenyezi Mungu
na tuweze kutarajia
kuokoka kutokana na haya maafa
tunayoishi nayo tangu pale tulipojitia katika
dhulma
kwa mikono yetu.
SERIKALI YA UMMA NDIO HAJA YA
UMMA
Matokeo ya uchaguzi wote uliofanywa Zanzibar tangu wa 1961
na mpaka wa 1963,
wa 1995 na huu wa leo 2000; yote
inaonesha na kuthibitisha haja ya Umma wa
Zanzibar kuwa
haja yao ni “Serikali ya Umma”. Umma wa Zanzibar
haukubali
kugawika mafungu mafungu, hata kama vitaletwa
vyama zaidi ya ishirini. Umma
wa Zanzibar uamuzi wao
ndio ule ule, tangu mababu, mababa na hata watoto, na
ndivyo
itakavyokuwa hata kwa wajukuu na vilembwe. Umma wa Zanzibar
ushaamua
na maamuzi yao ndio ya mwisho, haja ya Umma wa
Zanzibar ni Serikali ya Umma.
Wazanzibari hawataki kuzidi
kufarikishwa kwa kugawiwa vifungu vifungu.
Waliokuwa ZNP/ZPPP
ndio weshakuwa na waliokuwa ASP ndio weshakuwa. Ni wajibu
wa
ndugu zetu walioko katika uwongozi waikubali hali ilivyo na kwa
ilivyo
ndivyo twende, kutaka la muhali ni muhali; kutaka
Wazanzibari wabadilike ni
muhali na kwenda kinyume na matakwa
ya Umma ni kutaka muhali. Umoja wa
Wazanzibari muda wote
huo ulikuwa daima unalingania kuundwa Serikali ya
Umma,
kwa vile kufahamu umuhimu wake na kwa kutambuwa matakwa
ya
Wazanzibari. Umoja wa Wazanzibari uliendelea na unaendelea
kulingania
Serikali ya Umma mpaka hii leo.
SERIKALI
IMEFANYA MWANZO MWEMA
Alhamdulillah serikali chini ya uwongozi wa
ndugu yetu Bwana Aman Abeid Aman
imeanza kwa kuleta ishara njema
za kutaka kuleta umoja wa Wazanzibai kwa
hivi kuchaguwa Baraza
la Mawaziri ambalo linamathili zaidi uwananchi. Hii
ni
khatuwa njema ambayo ni busara kuipa mwega zaidi na kuiombea kheri
na
mafanikio. Lakini basi, itakuwa ni busara na kheri
zaidi iwapo Sheikh Aman
atachukuwa khatuwa zaidi
na kuwataka ndugu zetu CUF kuingia katika serikali
kwa
kuundwa Serikali ya Umma. Hapana shaka kuwa na ndugu zetu CUF
kwa
maslaha ya nchi yetu wataipokea khatuwa hio kwa moyo mkunjufu
na
kushirikiana na kufungua ukurasa mpya. Kama inavyoaminiwa na
wengi kuwa CCM
na CUF wanao kiasi ya 90% ya Umma wa Zanzibar
na kiasi ya 10% ndio sehemu ya
Umma ambo kwa ilivyo ni kuwa
wao hawana chama maalumu. Wote hawa ni wananchi
na wana Haki na
Wajibu sawa ambao ni lazima kutekelezwa kwa kushirikishwa
katika
serikali yao, hivyo ndivyo itakavyofanya hio “Serikali ya
Umma”,
serikali ya wananchi wote.
MASHAURI
JUU YA HIO SERIKALI YA UMMA
Kukhusu hio “Serikali ya
Umma” tunapenda kutoa raia kuwa iwe ya muda wa
miaka
sita badala ya miaka mitano, na kila upande upate fursa ya kuwa
katika
uwongozi wa Serikali hio kwa kipindi cha miaka
mitatu. Hivi kwa maana miaka
mitatu ya mwanzo kwa mfano CCM
ndio watakaochagua Rais na CUF watachagua
Waziri Mkuu. Na
baada ya miaka mitatu watabadilisha, CUF watachagua Rais
na
CCM watachagua Waziri Mkuu. Vilevile, ikiwa hio Serikali ya Umma
ina
mawaziri 14, basi sita iwe kutoka katika CCM na sita kutoka
katika CUF na
wawili kutoka katika huo Umma wa 10%. Hali hii
itawafanya wananchi wote
kupata kushirikishwa katika serikali
ya nchi yao bila ya ubaguzi kutokana na
fikra za kisiasa au
ubaguzi wowote ule.
KAMATI ZA UTENDAJI
Badala ya Waziri, ni
kuundwa Kamati ya Utendaji, kamati hizi zitakuwa badala
ya
Waziri; kwa mfano badala ya Waziri wa Fedha itakuwa ni Kamati
ya Fedha.
Kwa mfano kila Kamati itakuwa na wawakilishi
watano, wawili kutoka katika
CCM na watatu kutoka katika CUF na
Kamati nyengine itakuwa na Wawakilishi
watatu wa CCM na wawili
wa CUF, na kadhaalika. Wawakilishi watano hawa
wanne
watakuwa ni wanachama wa hio kamati yao na mmoja wao kati ya hao
wanne
atakuwa ni mwanachama na Katibu wa Kamati yao na watano wao
ndie ataekuwa
Mwenyekiti wa Kamati. Nyadhifa hizi zitakuwa
kwa kubadilishana kwa baada ya
kila muda. Mpango huu licha
ya kuwa utawapa Wawakilishi nyenzo ya
kuthibitisha uwezo wao
katika kutekeleza dhamana walizotwika na Umma
waliowachaguwa,
Umma unaotarajia upate utumishi wa Wawakilishi wao, bali
zaidi
utaondoa uwezekano wa ubadhirifu wa mali ya Umma na utumiaji
muovu wa
wadhifa na uzorotaji wa utendaji na
utekelezaji. Zaidi ya haya, mpango huu
utaleta
utaratibu wa kuwepo “collective responsibility and
accountability”
juu ya wote watakaoshiriki katika
utumishi wa serikali. Ikiwa ni sifa ni
sifa
ya wote, na ikiwa upungufu ni wote ndio wenye kuhisabiwa kwa
upungufu
huo.
SERIKALI YA UMMA HAIMUONDOI WA
ZAMANI
Kwa maumbile yetu, na kwa ilivyofanywa; kufika
katika madaraka imekuwa ni
njia ya kipato na njia ya
kujijengea fakhari na kiburi. Kutokana na hali
hii,
wengi wetu tunataka “kufa kupona” lakini nifike
katika utawala (na
nisitoke katika utawala) ili
niweze kupata chochote na niweze kuwa bwana
mkubwa,
niweze kutenda ninavyopenda bila suala wala jawabu. Niweze
kuchuma
(kwa njia ya haramu) kwa upesi kama nitakavyo weza
kabla ya kuondoka kwenye
utawala. Nihakikishe kuwa sitoki
katika utamu na raha hizi. Hali hii haiwezi
kufutika nyoyoni
mwetu leo au kesho, itachukuwa muda; muda ambao utalazimu
uwe
na mfunzo ya kuendelea na kudumu juu ya “UWONGOZI NA DHAMANA
ZAKE”.
Inahitaji tumjuwe na tumche Mwenyezi Mungu
katika dhamana ya uwongozi, hapo
ndipo tutakapoweza kupata
waongozi wa kheri, waongozi waaminifu. Safari ni
ndefu
kufikia huko, lakini penye nia pana njia – Inshallah
tutafika – Amin.
Kwa hivi sasa ni busara
kuwa bwana wa zamani awepo asipigwe pute mkate wake
na
bwana wa leo nae asinyimwe fursa ya mkate – madhali Umma
umewachaguwa.
Ilivyo ni kwamba Serikali ya Umma haimtoi wa
jana wala hamzuilii wa leo
kuingia katika utawala. Sote
tutakuwemo, kila mmoja atapata sehemu yake.
(kila mmoja
atabeba mzigo wake – mzigo wa dhamana za uwongozi –
hesabu
Kesho). Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu
atusaidie tuweze kujisaidia
katika utekelezaji wa
dhamana za uwongozi – Amin.
KUTENGENEZWA
KATIBA
Kwa kujikinga na uwovu wa uwezo (power) ni muhimu
ziwepo kanuni madhaubuti
za kuwahifadhi na kuwahisabu mabwana
wanaokuwa katika madaraka. Tusisahau
kuwa sisi ni binadamu
na binadamu ni mwingi na mwepesi wa kughurika na
tusisahau
kuwa: “power corrupts and obsulute power corrupts
obsulutely”.
Kutokana na hali hii ni dharura tuwe na Katiba
ambayo ina hifadhi haki za
mwongozwa na haki za mwongozi.
Katiba ambayo itabainisha na kuhifadhi “Haki
na
Wajibu” wa kila mmoja wetu kwa uadilifu kabisa. Katiba ambayo
haitaruhusu
yeyote yule kuwa juu ya kanuni, kanuni ndio
itakayokuwa juu ya kila kitu.
Katiba ambayo kwa haraka kabisa
itazifuta zile Sharia Ovu Arubaini zilizo
orodhishwa katika tume
ya Jaji Nyalali na kuhakisha kuwa hazitaletwa tena
katika
kanuni za nchi kanuni kama hizo au za mfano wake.
Kwa
kumaliza, tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ajaalie hii dhamiri na
nia
ya kuundwa “Serikali ya Umma” ithibiti
na itekelezwe kwa salama na amani kwa
manufaa ya vizazi
vyetu na jamii ya binadamu – Amin, Amin.
WA
BILLAH TAWFIQ
Umoja Wa Wazanzibari
Disemba 09,
2000
To subscribe to ZANZINET go to http://www.zanzinet.org/register.html
To
unsubscribe send "unsubscribe" command to: zanzinet-request@zanzinet.org
For
the list of ZANZINET members send "who" command to above
address