Author : Farouk Abdulla Amour
    Date: Fri, 23 Jun 2000
Subject: DHAMIRI NA ZENU NIA (MANIFESTO)

Nduguzetu,
Sheikh Seif
Sheikh Amani

Assalaam Alaaykum

DHAMIRI NA ZENU NIA (MANIFESTO)
Alhamdullilah, ni wajibu wetu kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hii nia 
yenu ya kufanya Serikali ya Umma.  Hapana shaka hili ndio muhimu na la 
mwanzo na ndio matakwa ya Wazanzibari kwa vile sote tunaamini kuwa hii ndio 
nyenzo pekee ya kuikoa nchi yetu – Mwenyezi Mungu akujazini kheri kwa nia 
yenu hii njema na akujaalieni tawfiq litengenee hili kwa manufaa ya vizazi 
vyetu na jamii ya binadamu – Amin.

Kufauatiana na nia yenu hii, hapana shaka muna mengi ambayo mushapanga kuwa 
ndio yatakayo kushughulisheni kuyatengeneza mara tu mukifika katika 
uwongozi, kwa maneno ya kileo huitwa “manifesto”.  Hapana shaka hamjapanga 
ila ni kheri juu ya kheri, lakini basi; ili na sisi nduguzenu na pia wazee 
wetu wayatambue hayo na zaidi wapate fursa na wao kuchangia rai zao juu ya 
hayo au yale ambayo huenda ikawa hamkujaaliwa kuyakumubuka, basi tafadhalini 
tuelezeni juu ya hayo mulioyapanga kuyatengeneza mara tu mukifika katika 
uwongozi.

Tunashirikiana kwa pamoja tunakuombeeni kila la kheri katika juhudi zenu za 
utumishi huu wa nchi yetu.

Wa Billah Tawfiq

Nduguyenu,
Farouk