Author : Faraj
    Date: Sat, 13 May 2000
Subject: HISIA YA SITA

Ndugu zangu Waislam
Assalaam aleikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh

HISIA YA SITA  (SIXTH SENSE) 'MILANGO YA MAARIFA'

Tunasikia sana juu ya hisia ya sita (Sixth Sense). Nini uhakika wake? Na
je, ipo kweli hisia hii ya sita?
Aristotle mwana falsafa maarufu wa Kiyunani amezihesabu Hisia (milango
ya maarifa) kuwa idadi yake ni mitano, nayo ni - Kuona kwa macho -
kusikia - kunusa - kuonja na kugusa. Zikapita karne nyingi na watu
wakasalimu amri kuwa njia za maarifa ni hizi tano tu.
Lakini baadhi ya wataalamu waliojitahidi kufikiri wakaanza kutafuta na
kutaka kujuwa juu ya hisia ambayo mtu wakati mwengine humjia akawa
anahisi kama kwamba jambo fulani litamtokea au litatokea, na wakati
mwengine likatokea kweli.
Wakaipa hisia hii jina la 'Hisia ya sita' (The sixth sense), hisia
ambayo wengine wameipa jina la 'Hisia ya ghaibu'. Lakini madaktari wengi
hawakubaliani na fikra hii ya Hisia ya sita, ingawaje wao pia hawakubali
kuzihesabu hisia au milango ya maarifa kuwa ni mitano tu, kwani nao
wamegunduwa kuwa mwanadamu anahisi kwa njia nyingi sana kuliko idadi
hiyo. Wao wanahesabu mtu anapohisi njaa kuwa nayo pia ni katika Hisia,
na pia anapoona kiu, au zile hisia za juu ya ngozi. Wao wanasema kuwa
ngozi haihisi kwa kuguswa tu, na hii ni baada ya kugunduwa kuwa katika
ngozi mna mishipa ya fahamu (nerves) mingi sana.
Kwa mfano pana mishipa inayohusika na kulihisi joto tu, na mingine ya
kuhisi baridi tu na ipo ya maumivu  na mingine inayohisi pale inapoguswa
nk..
Kwa ajili hiyo hisia ya sita haitambuliwi kabisa katika ulimwengu wa
matibabu.

(IMENUKULIWA KUTOKA KATIKA KITABU 'KILA SUALI  LINA JAWABU YAKE'
KILICHOANDIKWA NA MUSTAFA ASHUR)

Wassalaam aleikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh
Ndugu yenu
Muhammad Faraj Salem