.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Shilingi In-geleka

 

 

 

 

 

 

Related links

 

Shilingi In-geleka!

27 Feb 2000

 

Wenzangu nawakumbusha, kuhusu hii shilingi,
Jana neipata machumini, kazini nlikokuwa,
Haiweka nfukoni, nkenda zangu nyumbani,
Shilingi in-geleka, chakukila sitimizi.

Kutwa jana nehangaika, majasho yakinitoka,
Roho ilinikauka, shilingi ndo haipata,
Nikaingia nyumbani, mchagoni haiweka,
Shilingi in-geleka, chakukila stimizi.

Nemka unjuye, nje nikajiendea,
Nikafanya la kufanya, kisha harudia ndani,
Nkenda mchagoni, kuifuata shilingi,
Shilingi in-geleka, chakukila sitimizi.

Hamwendea baba yangu, kumpa hii habari,
Akasema kanechoka, na shilingi isodumu,
Akanipa yake rai, niache kuitegemea,
Shilingi in-geleka, chakukila sitimizi.

Kasema niache kazi, nfanye yangu mwenyewe,
Itakuwa na thamani, na hadhi ya kusifika,
Itaimarisha nyumba, mashaka konokea,
Shilingi in-geleka, chakukila sitimizi.

Mie hii shilingi, yanichosha maboye,
Bora nimsikilize baba, kazi nianzishe,
Ntapata yangu shilingi, kamwe haitageleka,
Shilingi in-geleka, chakukila sitimizi.

 

Mtungaji:

Mohammed al-Nabhany

B.A - E.L

Toronto

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet