|
|
Jinga Leo ni Jerevu!
Date: 06 Feb 2001
-
Jinga lilikuwa kale, zamani za ulegevu
Jinga lisikae mbele, ya watu kwa upumbavu
Jinga lierevushile, kwa mambo yenu maovu
Jinga leo ni jerevu, hilino si jinga tena
Muyaka Bin Haji
Limeletwa ukumbini na Ibrahim Noor
|