|
|
Kioo!
Date: 22 Mar 2001
Kioo kinapumbaza, wangapi wapumbazika
Wengine kinawalaza, namajoho kuwavika
Sifa yake miujiza, viumbe waathirika
Kuwa wewe kwenye kiza, kauli umeumbika
Wengine hukiapiza, miko machozi kutoka
Chatowa jina aziza, wendako unasifika
Simdogo siajuza, wote kwake malaika
Chakupamba chakuliza, wanguruma mwananyika
Wajinata chakucheza, kumbe unamungunyika
Kioo kukichunguza, wateleza wachujuka
Hashil
Kioo!
Date: 22 Mar 2001
- Kama ukaninunua, Hajazo hakufanyia
Penye kovu hakwambia, Tena ukazingatia
Jipulo ukalivizia, Na uso ukajikwabua
Kioo nakukosa nini?, Hebu nifafanulia
- Sinalo lakuzidisha, Ulivyo ndivyo najua
Tena hakukumbusha, Usowo matongo sikia
Tena hakuamsha, Upendeze kwa yako njia
Kioo sinitie makosani, Bwana nakuangukia
- Hivyo upewe kisu, Ukamchinje ngamia!
Halafu useme usu, Bora nimchinje Rabia
Hilo sikosa la kisu, La wewe ulivyoamua
Kioo yanihusu nini?, Kosa ni lako sikia!
- Amkeni waungwana, Muitizame dunia
Makosa kutupiana, Na lawama kila njia
Si mtu huwa avuna, Alichopanda, sheria?
Kwa makosa siyaoni, Kumbuka ulivyonitumia.
Ali Rashid Salim
|