Mapambano!
Date: 31 Mar 2001
Damu haishi mwagika, kama mvua masika
Nyoyo za watu zalika, shida zinawamurika
Kila wanalolishika, limoto kukamatika
Humuuliza hakika, mpaka lini Rabuka?
Muumba ametupika, nusu njia sikufika
Safari yetu ya nyika, muhanga ndio hakika
Tujifunze kuzishika, msimu utapofika
Kwaherini nakatika, jikoni niko napika.
Hashil