.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

MPAKA LINI ?

 

Related links

 

MPAKA LINI ?

Date: 21 May,2001

  1. Ulimwengu washangaza , mabingwa unawazuga
    Sifaze wabembeleza , umma kutwa washilanga
    Kazi kubwa ni kucheza , jina la ngoma kisanga
    Kivumbi kitapoanza , kondeni shoka na panga.
  2. Pingu zafungwa akili, kuzifungua mashaka
    Yakufanya ni mawili , khofu kwanza kuizika
    Lapili kujisajili , tujuane pakusaka
    Wakati ukiwasili , tupambane na majoka.
  3. Kitandawili natowa , jawabu nalingojea
    Simba kaliwa na ngawa , vinyama vikasogea
    wakaanza kuchagawa , kadhia ilotokea
    Kisa kinanisumbuwa , nimebaki naelea.
  4. Nyoka waajabu , duniani ametua
    Kiya lake la dhahabu , na miguu ya shazia
    Chakula chake zabibu , hakuna asiejua
    Sumu yake inatibu , magonjwa yanosumbua.
  5. Malumbano si mshoto , wakuchokorea pweza
    Madhumuni siyo joto , chuki kuzitapakaza
    Njugu zafanywa kokoto , mshipi wakurambaza
    Twapakana manukato , kama hina ilokoza.

Hashil S. Hashil

 

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet