.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Mwana Msambe Dhihaka

 

Related links

Mwana Msambe Dhihaka

Date: 25 October, 2001

  1. Mwana msambe dhihaka, ni majani ya ukoka, tuyatunzeni.
    Mwana kito kitukuka, ugomvi tumeshachoka, tuuateni.
                     Mwana msambe karaha, tumtunzeni.

  2. Mwana mwokovu fahali, tumtunze mwanamwali, zingatieni.
    Mwana habibu kauli, tusikubali kitali, tahadharini.
                     Mwana msambe karaha, tumtunzeni.

  3. Paka shume lavinjari, letoroka guniani, tukumbukeni.
    Hasidi wa mwanamwari, hamtaki muhisani, mfukuzeni.
                      Mwana msambe karaha, tumtunzeni.

  4. Kelele za mlangoni, mwenye nyumba burahani, tutambueni
    Halahala na matoni, hoho imo ujitini, ikimbieni.
                      Mwana msambe karaha, tumtunzeni.

  5. Si usiku si mtana, kula kunywa usimama, wa hamkani.
    Mwari sasa si usena, kuchoma kutafunana, tukuateni.
                     Mwana msambe karaha, tumtunzeni.
  6. Muungwana ni vitendo, fadhila tukitendewa, tushukuruni.
    Hongera kwa huu mwendo, mwari akishaolewa, tufurahini.
                     Mwana msambe karaha, tumtunzeni.

Ahmed Rashid

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet