.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Nasaha!

 

Related links

 

Nasaha!

16 Dec 2001

  1. Laana, kuteremkia watu, kwanza awali, hunyosheana vidole
    Bayana, wakaondosha na utu, hata wawili, hupigiana kelele
    Uwana, kwa panga na mirututu, si mbali, huyu kuuwa wa yule
    Maana, dhaifu imani zetu, na dalili, kwa bayana twaziona

 

Ibrahim Noor

 

Nasaha!

17 Dec 2001

  1. Laana, ada ikifurutu, wenye akili, hugeuka wapole
    Hiyana, ya mtu na mtu, huhasiri mali, tele wa tele
    Amana, za wingi wa vitu, vya asili, na vya kale
    Maana, uchafu wa roho zetu, na dalili, kwa bayana twaziona.
  2. Laana, viamboni na misitu, hukalili, ukubwa wa makole
    Hakuna, cha kujaa upatu, cha kumtosha fahali, wana na wavyele
    Hasana, hairudi katu, na kusema kweli, haitarudi milele
    Maana, ufisadi wa nyoyo zetu, na dalili, kwa bayana twaziona.
  3. Laana, yazidisha papatu, ikaondoa adili, pole pole
    Hapana, anayethubutu, kujifanya dalali, akatoka mbele
    Amina, ewe mola wetu, twaomba jamali, na utuongole
    Maana, hafifu ibada zetu, na dalili, kwa bayana twaziona.

 

Kassim O. Ali

 

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet