.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Tamu ya Wali!

 

Related links

 

Tamu ya Wali!

18 July 2001

  1. Si lazima kwa mchuzi, ladha wali kuibaini
    Pilau kwa nyama mbuzi, inapikwa majumbani
    Na wapishi wamaizi, huipamba biriyani
    Tukawa hatujuwani, tonge vinywani hujazwa

  2. Kuna na wali wa kamba, ladhaye hujaijuwa
    Na kwa cha bwana-kilemba, mchicha au mayugwa
    Sifaze nitaziwamba, wajuwe wasozijuwa
    Sufuria wakanguwa, Mkonowo wauramba

  3. Mkonowo wauramba, kipikwa ukapikika
    Kitumbo kikavimba, lepelepe hukushika
    Huchelei na kuyumba, hadhara waaibika
    Bara-Hindi hadi Pemba, Nyali hujazila nyali

 

Ibrahim Noor

 

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet