|
|
Upo Upo Hapo?
Date: 5 April 2001
- Nasikia kuna kitu, jina lake umekwisha
Nahalafu kuna mwitu, jina lake unataisha
Nenda zako huna kitu, machachari yasokwisha
Nipishe mzee chatu, kazi yako kuulisha.
- Mama mwanawe ataka, maziwa kumnyonyesha
Alia mithili paka, namachozi yanamwisha
Vurumai na mashaka, ndiyo yanomuyayusha
Kijiwe kinampaka, tumechoka kukodisha.
- Siti rejea nyumbani, nyimbo zako zasifika
Zikitutia imani, kila kipembe zafika
Umebakia moyoni, kishada kilotoweka
Lakufanya liko pwani, kuyoyoma kujizika.
- Penye wengi panamengi, tusijifanye vizoro
Porini kuna shilingi, na pia makorokoro
Posimo mimi gingingi, mambo hayo ni uharo
Paparika hutupingi, ni njia ya che.kovaro.
Hashil
|