Usiku wa Mwisho!
13 Dec 2001
Ile ndoto kwenye kiza ~ Imefunikwa na Nuru
Nimeota muangaza ~ Na mikono Nashukuru
Mola Naomba jaza ~ Huo moto Ninusuru
Macho Nimefumbiza ~ Sinao tena Uhuru
Naona Ya kushangaza~ Mola wangu ya Ghafuru
Mie kwako mejiteza ~ Ya Awalu ya Akhiru
Nazidi Kukutukuza ~ Jina lako Nadhukuru
Nayo mema kufanyiza ~ Nizidishie umuru
Niwe kwako Napendeza~ Mauti yakinidhuru
Hadha Ru'aya fawaza ~Allhumma ya khabiru
Warehmatika waljaza ~Waneematika Ashkuru
Ya Karim ya Aziiz ~Wal sauma Thawaba Takthirru
A.BAJA