.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Vitendo si Maneno

 

 

 

 

 

 

Related links

Vitendo si Maneno!

Date:  14 May 2001

  1. Aitafuta bahati, amezugwa na wakati
    Alitakalo hapati, kaibuka na machati
    Kwao hataki kuketi, ati hakuna gazeti
    Bado yeye mwenye kiti, atuna kuliko seti.
  2. Pendo ni sumu ya nyoka, viumbe kuliepuka
    Lakukumba wachujuka, umwehu wakugubika
    Waenda wamungunyika, wasomacho wakucheka
    Dawaye ni kuzinduka, Au utaathirika.
  3. Matusi kwao ni ngao, matunda wayachumayo
    Limbukeni nyendo zao, kutwa ndiyo hayo hayo
    Nimchwa kwenye ubao, ufisadi mambo leo
    Husuda ni chombo chao, abiria vyoo vyao.
  4. Tatizo ukiwanalo, kutanzua ni mazao
    Hutafuti kubwa lao, kukwepa uliyonayo
    Wasimama na mrao, kuzizima chuki zao
    watafunga kwenda kwao, watabaki mshangao.

 

Hashil S. Hashil

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet