|
|
Juma Duni Ongoza Nchi!
Date: 24 May 2002
- Juma Duni ongoza, mapambano hadi mwisho
Ukae na wako wenza, Maalim na Profesa
Na Mloo aso inda, na vingangari vitoto
kitabu tumekisoma, na maana imetinga.
- Tumshukuru Vairasi 99, bila kiasi
kututilia irabu, ya yale ya Juma Duni
Hivyo nani atabisha, ALLUTA KONTINUA
Uzanzibari sawia, wala sio Uafrikia.
- Huu Uafrikia, hapa ndipo ulipotufikishia
Madhila yaso na njia, kwa hakika yametungia
Nchi twaikimbia AAAH!, Sababu ya Mchonga pia
Laa hapa basi nakwambia, mbugani tuzidi ingia.
- Nyote Wazanzibaria, Umoja wetu ndio njia
Tukijatena regea, hakuna wakulaumiwa
Sote miguu sawia, vita hii kumalizia
kuanzia Canadia na Uingereza pia, Dr.Hassan usijekimbia.
- Mollah bariki njia, ya Umoja Wazanzibaria
Tusijetena chafuliwa, na vibaraka wasonjia
Tupate zetu afia, na Uchumi kuinua
Tamaduni kuzisimamia, zile zetu asilia
Ya Rabbi Dua Taqabalia.
Wasalaam,
Ally Bin Aboubakar,London.
|