|
|
Kwaherini!
Date: 11 Apr 2002
- Shairi langu la mwisho, Nakuageni wenzangu
Kutunga kuna uchosho, Zimekwisha beti zangu
Labuda mwaka kesho, Udumu uhai wangu
Nitaleta ukumbusho, Faida kwako na kwangu
-
Moyoni ninasumbuko, Kwaheri ina machungu
Fikira huko nendako, Zimetanda ulimwengu
Kutunga kuna miiko, Vina fungu kwa fungu
Kwaherini jumuiko, Wakati si mali yangu
A. BAJA
|