.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Pambo Lake

 

 

 

 

 

 

Related links

 

Kutoka kimbuga (shairi la pambo lake)

Date: 23 May 2002

Mai yanayoelezwa, yachomoza milimani
Kuja kwake kwa muruwa, na nyimbo za wastani
Utamu wake haluwa, wajiramba midomoni
Nivigumu kutambuwa, wenye macho hawaoni.

Chombo chake si mtungi, si debe wala sahani
Rangiye zaafarani, mywaji awa angani
wengine wao hulani, wakati wako ghalani
Kiumbe huwa shetani, kisuche huwa kwapani.

Maji hayo ni adhimu, wayapata uvitani
Mara unapata pumu, nakuita maruhani
Wajikuta usanamu, ufukweni unaghani
Mawimbi yake ya sumu, si ya nyoka si nyani.

Wakatabahu
Hashil

 

Date: 23 May 2002
Kutoka kimbuga(shairi la pambo lake)

Nami nidokeze langu, ya mai kuyaeleza,
Hayakuuzwa ja changu, lilamu kuyasambaza,
Mai yamtoa pingu, masikini kumkweza,
Si jura si Mfalume, kwake ni kito adhimu.

Wengine huyaghania, mai matamu ajabu,
Wengine huyavizia, mai hayo mahabubu,
Wengine huyaotea, mai mema kwa kutibu,
Si jura si Mfalume, kwake ni kito adhimu.

Si vigumu kutambua, Bw. Hashili baini,
Bongo mtu kifungua, humuingia yakini,
Na mai akiyajua, moyo uko taabani,
Si jura si mfalume, kwake ni kito adhimu.

Ahmed rashid

 


 

 

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet