.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Shairi Fumbo

 

 

 

 

 

 

Related links

 

Shairi Fumbo!

Date: 28 Nov 2002

  1. Washairi karibuni, Salamu zangu natowa
    Wabara hadi wapwani, Walamu na wakiluwa
    Nimeshindwa kubaini, Moyoni la nisuguwa
    Kendacho hadi angani, Charuka bila mbawa
  2. Meuliza mafanani, Vitabu wakafunguwa
    Na waalimu wazamani, Na shahada ziso dowa
    Wameshindwa kubaini, Bure mnimejisumbuwa
    Kendacho hadi angani, Charuka bila mbawa
  3. Hakitumii mashini, Au nguvu za sola pawa
    Wala hakina rubani, Kama meli au mashuwa
    Fundi umeamuani, Umeweza kukijuwa
    Kendacho hadi angani, Charuka bila mbawa
  4. Sikusaza arabuni, Nao nimewashituwa
    Na khsa hapo omani, Ni wengi naowajuwa
    Washairi wa zamzni, Ujuzi usopunguwa
    Kendacho hadi angani, Charuka bila mbawa
  5. Mji wa kwenda yemeni, Fumbo msipo lifumbuwa
    Nina sahiba fulani, Moyoni sitomondowa
    Nasikia taabani, Maradhi yanamsumbuwa
    Kendacho hadi angani, Charuka bila mbawa

 

Beit-alajaeb

 

Shairi fumbo

Date: 29 Nov 2002

    Mauti mja yakija, mashaka humuingia.
    Kendacho hadi angani, Charuka bila ya mbawa.
    Mauti haki kwa mja, hakuna wa kukimbia.
    Kendancho huko mbinguni, kama livyoahidiwa.
    Roho huruka angani, bila mbawa mar'ia.

 

Ahmed Rashid.

Shairi fumbo

Date: 29 Nov 2002

  1. Usipate taabu mno, zamani nalisikia.
    viko vingi vyenye vuno, navyo vina jirukia.
    yalete mengi mavuno, tupate kualikia.
    Lete na vitafunio, bashrafu kuanzia.
  2. Ni vingi havina mbawa, navyo vyajipururia.
    lete kwa rangi na sura, tupate kuchagulia.
    isiwe kutuburura, hapo hutaambulia.
    hatutanasabu chura, tukatoka na ngalamba.
  3. labda mtu mbumbumbu, jawabu takupatia.
    kwa hapa kwetu bububu, kapuni tutalitia.
    kwani hilo fumbo butu, halina pa kuanzia.
    tena sio la kiutu, kwani linasinzia.

 

Walii Genderi.

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet