.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

SI UBETI WANGU

 

Related links

SI UBETI WANGU

Date: 27 Dec, 2002

    Wambaje mwenye kutamba - Pahala pa kivuuko
    Na ntoni muna mamba - Pwani ntumbwi hauko
    Akakutokeya simba - Akakutisha vituko
    Utakwenda kwenye simba - Au tangiya ntoni ?

Saleh Barkey

SI UBETI WANGU

Date: 27 Dec, 2002

    Sitaingia ntoni, kuhatarisha maisha,
    Mamba yeye yu nyumbani, hata nvua kinyesha,
    Simba tu wote ugani, akitisha tantisha,
    Tanrukia shingoni, ntoni kunivuusha,
    Nitarukia ntini, kusalimika si hasha,
    Nahisi upunguwani, ntoni kujizamisha,
    Sitaingia ntoni, kuhatarisha maisha.

Ahmed Rashid.

SI UBETI WANGU

Date: 28 Dec, 2002

  1. Ntambaji yuabesa, Ingawaje hana pesa
    Yungali apwesa pwesa , Jawabu ameikosa
    Mamba roho anitesa , Aona hivi yatosa
    Nako huku kuna visa , Hataki mpa furusa
  2. Nti hiuparamiya, Simba tawi tarukiya
    Kukavu kikimbiliya, Mamba tanifukuziya
    Harufuye yanukiya , Wawili wananijiya
    Dawa ni kunrushiya , Mafinge kumtupiya

Sayed Al Mugheiry

SI UBETI WANGU

Date: 29 Dec, 2002

  1. Sibesi sinakutamba, nimekwama kivukoni
    Si wasimba si wamamba, natetemeka pembeni
    Kitafakari kiomba, japo simba simuoni
    Yake sauti mepamba, ikinguruma mwituni
                    Naogopa taabani
  2. Nimebakia na mamba, twatizamana machoni
    Mdomo mwili kavimba, kajizamisha majini
    Akisikiza ya simba, sauti kiwa mtoni
    Hanajicho alofumba, ndotoye nishuke chini
                   Nami ng'oo,darajani
  3. Simba akajitokeza, kumuona kama ndama
    Mambo yakanishangaza, sikuwa na lakusema
    Vituko alivyofanza, kunitisha kunguruma
    Njia tukaiogoza, simba mbele mimi nyuma
                   Mamba mtoni akema
    1. Maher Fundi (Unique)

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet