|
|
Ubani!
Date: 11 Apr 2002i
- Mwenzenu nauzwa swala, Jawabu nileteeni
Nipeni japoishara, Linituwe akilini
Ubani tamu kuliwa, Raha yake ndio nini
-
Yamenisibu madhara, Nikiukosa mashakani
Katu sendi pahala, hakutokeki hadharani
Nikikosa bila kula, Daima sijiamini
-
Naogopa Nikaraha, Mwenyewe nasema moyoni
Kuacha pia madhila, Sipendezi Uwanjani
Kutafuna nikiula, Ubani ni ladha gani
-
Meno yanapishana, Mara juu mara chini
Ulimu mtamu sana, Ladha yake siioni
Tabia kuchakuana, Tamu yake nambieni
A. Baja.
|