|
|
Alolala usimuamshe,utalala wewe
Date:15 Jan 2003
- Utamu wa kutawala, unawatia wazimu
Waamka wakilala, mume mke wako zamu
Haamshwi alolala, jambo hilo ni muhimu.
- Kiwera kiloingia, kitafuteni wenyewe
Ziko nchi zawambia, serikali waiuwe
Halafu kuzingatia, kushirikiana wajuwe.
- Mgogoro umondani, Amani hajitambuwi
Salmini hamkani, leo sefu si aduwi
Amejigeuza nyani(salmini), kumbe mwenzetu ni chuwi.
- Wang'olewe kwa mizizi, tuwazomee ujima
Lakutafuta ni ngazi, tuwe juu wako nyuma
Wengi wao leo chizi, kutwa wamo kuungama.
- Adabu yao kuimba, ngoma iwe ni marimba
Mtoni tutie mamba, masikio tia pamba
Wote tuwafungé kamba, kuwatia jamba-jamba.
Hashil
|