.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Chemsha Bongo

 

Related links

Chemsha Bongo

Date: 23 May, 2003

  1. Kila kitu kina mwisho, usingie ujingani
    Uonacho mzungusho, hiyo pia iangani
    Wengine ni vichekesho, mabotea ya jangwani.


  2. Ujuacho huwa sicho, vigumu kuweza juwa
    Vingi vyao ni mficho, yatakiwa kupembuwa
    Yatakiwayo ni macho, na moyo usonadowa.


  3. Mbweko wa mbwa koko, hauzuwii wendako
    Wakumbuka ya viboko, watizamaji vicheko
    Bado wao chokochoko, majikoni ni mpiko.


  4. Yakuishituwa cheche, uwanjani kuingia
    Asotaka umuache, hakuna kumzingia
    Masikini ndugu Che, yako mengi kachangia.


  5. Leo hili kesho lile, konde yao inamwitu
    Matunda yao kelele, kugombana kwao utu
    Hatua kumi za mbele, mia za nyuma ni kutu.

Hashil

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet