|
|
CHOZI
Date: 30 March, 2003
- Wapi linapotokea, wapi linapoanzia
Ikiwa chozi hisia, huwaje ukalilia
Usoni kudondokea, machoni linotokea
Unaumwa waumia, kwa wivu wako tuliiiiaaaaaa!!
- Ni chozi arukaruka, mbawa nitazikata!!!!!
Kama ndio washauka, kutaka kuyafuata
Machozi yatakutoka, utafute wa kufuta
- Chozi kwa wangu mpenzi, ni MAHABA huyavizi
Chozi la HUBA la ENZI, lenye utamu wa ndizi
Chozi kwa wangu AZIZI, chozi si kwa wewe MWIZI.
Salma Khamis (Chama).
|