.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Waridi

 

Related links

Kabla ya Macho Yangu

Date:  16 June 2003

  1. Naomba siniamshe, niwache usingizini
    Ndoto niikamilishe, kiwa kwako ubavuni
    Wala sinikurupushe, ikaniruka kichwani
    Nisaidiye isishe, nionayo niamini

  2. Nilikuona zamani, kabla ya macho yangu
    Ukabakiya moyoni, huku nikiomba Mungu
    Nikutiye mikononi, nikupe umri wangu
    Leo hii naamini, siku imefika kwangu

  3. Tumevaana mwilini, kwa shauku na furaha
    Mioyo iliyo ndani, yatupiga na kuhaha
    Kigongana kifuani, na pupa isonasiha
    Tukipeana hanani, mapenzi yalo na raha

  4. Uzuri mithili yako, sijaona duniani
    La fakhari umbo lako, na urefu wastani
    Unang'ara uso wako, kama mwezi wabaini
    Napenda bashasha zako, ucheke nnatamani

  5. Sura yako nimevikwa, imenijaa machoni
    Sitokubali kushikwa, kuumizwa zangu mboni
    Takulinda hutofikwa, paziya lako kopeni
    Yatapokuja pofukwa, wewe utakuwa ndani

          Salama huonekani

 

Maher

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet