.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Kikulacho Kinguoni Mwako

 

 

 

 

 

 

Related links

Kikulacho Kinguoni Mwako!

Date:  28 Sept 2003

  1. Kweli akili ni nywele,kila mtu ana zake
    Kweli akili upele,huja na muwasho wake
    kweli akili kengele,hugonga kwa saa zake
    Si mageni yako tele,hupita kwa njia zake.

 

John Smith

Kikulacho Kinguoni Mwako!

Date:  29 Sept 2003

  1. Akili huwa ni mbili, moja huwa siyo yako
    Akili kitandawili, wakiteguwa wenzako
    Akili ni pilipili, muwasho andasazako
    Akili kama tumbili, yachupa mitini kwako.
  2. Asali utamu wake, haiishindi shubiri
    Asali ni peke yake, yakufanya ufikiri
    Asali chumvi mwenzake, wajikuna utitiri
    Asali ni sega lake, waulizwe wanawari.
  3. Kikulacho kinguoni mwako, jambo hilo si kicheko
    Kikulacho kaka yako, barazani ni vicheko
    Kikulacho huwa wako, sihasha ni baba yako
    Kikulacho huenda hakiko, wasiwasi nyendo zako.

Wakatabahu

 

Hashil

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet