.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Kizungunkuti

 

Related links

Kizungunkuti

 23 Jan 2003

  1. Tafadhali niambie, usiniweke kizani
    Akili pate tulie, nijue nasema nini
    Mafumbo sinipigie, kunitia hamkani
    Mwezangu nitamkie, wewe kiumbe gani


  2. Machozi yako yaweke, wala moyo sishituke
    Mwenzako bado ni pweke, mekusabili niteke
    Wala usihangaike, mkono wangu nishike
    Kheri yangu utamke, majonzi usiyaweke


  3. Umenitia kitanzi, sijui kujitanzua
    Zimenijaa pumzi, wala siwezi pumua
    Na wewe si muokozi, hajayo kunisumbua
    Yareti ungemaizi, hadharani kukujua


  4. Hukuvuta nifulani, ambae ametoweka
    Hukudhani ni mwandani, moyoni nilokuweka
    Nisaide ni nani, mwenzio ninateseka
    Nakuomba samahani,  kalamu ninaiweka

          Miminae

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet