.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Malkiya

 

 

 

 

 

 

Related links

Malkiya

Date: 05 September, 2003

  1. Nipe vyako zamani, ambavyo nimezoweya
    Nivienzivyo moyoni, kuvikosa ni udhiya
    Vya wengine sivioni, ya kwamba vimetimiya
    Nambie nifanye nini, mimi kwako maridhiya

  2. Umbo lako wastani, Ndilo linonivutiya
    Ulopewa na manani, kweli kakuchaguliya
    Haiba na zako shani, zazidi kupaliliya
    Mwenginewe sitamani, hata kumuangaliya

  3. Kikwita Huruaini, bado nakupunguziya
    Ujuzi na zako fani, Katu hawajafikiya
    Umepasi mitihani, wao waloikimbiya
    Kitiwa mwao kundini, wewe kwao malikiya

  4. Mpenzi usinihini, juwa kwako naumiya
    Hutoki mwangu ndotoni, Na kutwa nakuwaziya
    Usidhani ni utani, Haya ninayokwambiya
    Ukija kunizaini, Juwa nimeangamiya

Anonymous-146

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet