|
|
Mama Zanzibar!
Date: 15 Feb 2003
- Umezaa na kulea, wengi mno auladi
Kubagua hukujua, ndani ya mwako fuadi
Huku kiwakumbatia, kuwalinda na hasidi
Baraka kiwamwagia, kuwafanya mashadidi
- Siku mpya kingia, kukuta kwenye jihadi
Sio jua si mvua, lokukata juhudi
Mengi mevumilia, wewe kweli ni shahidi
Mabungo tukijilia, hakika tulifaidi
- Wengi tumekukimbia, Tumehajiri biladi
Dunia tumeenea, Tumezivuka hududi
Si kwamba twapendelea, twakimbia ufisadi
Ni lini tutarejea, Ajuwae ni wadudi
Said Paul
|