|
|
MASHAIRI YA MAPENZI
Date: Date: 28 May, 2003
- Mapenzi kitu ajabu, yakutia bumbuwazi
Yakufanya uwe bubu, kujibu huwa huwezi
Shubiri kwako zabibu, na vitamu huviwezi.
- Wamkuta kaemewa, asemayo hayajuwi
Aumba akiumbuwa, aona maruwiruwi
Vigumu kumuopowa, na kwa ngisi kumvuwi.
- Hukumbuka ya zamani, yote walofanyiana
Nyumbani barabarani, ayaona kama jana
Akili yake ya nyani, aruka inagongana.
- Wangoja nyota ya jaha, kutwa wewe unahaha
Mawazo yako silaha, akukwaaye usaha
Usifanyiwe msaha, waugeuza karaha.
- Kalelewa kaleleka, utani kwake ni mwiko
Njiani yeye na kaka, hapokei mualiko
Ghadhabu zake za paka, hapendi maziko.
Hashil S. Hashil
|