.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Mkondo wa Mashairi

 

Related links

Chemsha Bongo Kwenye Mkondo wa Mashairi

Date: 22 Juni, 2003

  1. Uchaguzi ni daraja, tujizatiti kikweli
    Mke mume na mkaja, njia zote za halali
    Ushindi utapokuja, imani siyo ukali.


  2. Kafukuzwa kiidhara, wenziwe midomo wazi
    Jina lake ni kachara, abwabwaja kama chizi
    Huko nyuma akingara, leo mithili jambazi.


  3. Waanguka wanyanyuka, na hatuwa wazidisha
    Hujifanyi kama paka, na macho kuyarembusha
    Hakuna lisoshindika, onyesha zako bashasha.


  4. Nchi zote katataga, hakupata atakacho
    Wamuona anaaga, hakuangalii macho
    Atafutiwe waganga, wamtibu kimlacho.


  5. Hunijui sikujuwi, tatizo sijalijuwa
    Ikiwa mwenzagu chuwi, mimi kuku naanguwa
    Naambiwa ni kiziwi, dunia yanisumbuwa.

Hashil

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet