.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Moyo Usio Kinai

 

 

 

 

 

 

Related links

Moyo Usio Kinai!

Date:  06 Oct 2003

  1. Nilidhani nimepata kumbe nimepatikana
    Kitowa pasi matata kukuridhi muungwana
    Kumbe bure najinata mwenzangu habari huna
    Kila nikifurukuta wataka tena na tena
  2. Mchango kuchangizana moja na moja ni mbili
    Na sio kuumizana mwengine kuwa bakhili
    Iko kuchukuliana pale panostahili
    Unapoleta khiyana Ishakuwa mushkeli
  3. Nilikupa kila changu shaka sikukutiliya
    Kwa kujuwa umwenzangu Katika yangu duniya
    Kumbe vile ulimwengu ulikwisha kuchezeya
    Meniachia machungu vigumu kuelezeya

 

Said Paul

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet