|
|
MPENZI WANGU(1)
Date: 1 March, 2003
- Nijuvye mpenzi wangu, hali yako ulonayo
Zimepita siku chungu, sijasikiya haliyo
Hukaribu chini yangu, nikapoza huu moyo
Naungulika kwa hayo
- Waniruka usingizi, kucha nikikufikiri
Hebu itika laazizi, iondowe yako ari
Siku naiona mwezi, lazima kweli nikiri
Naiogopa kwaheri
- Kama uko ugonjwani, nambie nije haraka
Nitafute chombo pwani, au ndege ntaruka
Nifike kwako ayuni, roho itafurahika
Niondowe yangu shaka
- Lau kama nimekosa, nikheri uniambie
Hivi sasa wanitesa, dhiki naijuwa mie
Sina moja la anasa, nimekonda kama sie
Mwenzio nihurumie
Salma Khamis.
MPENZI WANGU(2)
Date: 1 March, 2003
- Mpenzi wangu itika, mapenzi yako hakika.
Pekeo nilokuweka, moyoni umefungika.
Mbona wanipa wahka, Mpenzi nilokutaka.
- Anga nikiiangaza, macho yananiongoza
yako inayong'aza, sura yanipumbaza.
Kila nikijikaza, nashindwa wangu aziza.
Salma Khamis.
|