.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

MUHOGO WA JANG'OMBE

 

Related links

MUHOGO WA JANG'OMBE

Date: 25 August, 2003

Kiitikio:

  • Muhogo wa Jang'ombe, sijauramba mwiko
    Usitukane wakunga, na uzazi ungaliko
  1. Kaditamati naapa, muhogo sitonunua
    Haikuwa Maimuna, aliyekwenda ung'oa
    Kapata tete kuanga, na ugonjwa wa shurua


  2. Kula dori kula dori, mshindo wa sufuria
    Guliguli guliguli, kofia ina viua
    Ndiye mimi ndiye mimi, anipataye ukoa


  3. Mungu akitaka kupa, hakuletei barua
    Hukupa usingizini, pasi mwenyewe kujua
    Kwenda mbio sikupata, bure unajisumbua


  4. Mkato wake matege, wakati anapokuja
    Naliiweka dhamiri, ya kumfulia koja
    Wallahi nimeghairi, kiumbe hana mmoja


  5. Kamfunge kamfunge, beberu wa Athumani
    Umfunge umfunge, pahala panapo jani
    Endaye tezi na omo, atarejea ngamani


  6. Sina ngoa sina ngoa, kuhadaiwa sitaki
    Ni mwerevu ni mwerevu, wala sihadaiki
    Pambanua pambanua, viwili havipendeki


  7. Ya nini kutakadamu, kwa jambo lisilokuwa
    Utahadhari na mwiko, wakati wa kupakua
    Ukitamani makoko, chungu utakitoboa


  8. Nauliza masuala, hamnambii jamani
    Watu wake wakishiba, huzidi umaluuni
    Pahala pasipo ngoma, hupandwaje na shetani

Nyimbo ya Bi Kidude
Imeletwa na Hassan O. Ali

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet