.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Mwana wa Moyo

 

Related links

MWANA WA MOYO

Date: 1 May, 2003

  1. Mama kimwana wa moyo, najiuliza kwa nini
    Kitwetatweta mlio, katu sijayaamini
    Sauti ghafla hiyo,  gharib masikioni
    Mwana naumia moyo, hayo sikuyadiriki.


  2. Mbali ya uoni wangu, angavu siikadiri
    Mumba ardhi na mbingu, kadiri yake Bashiri
    Mama huu ulimwengu, ninauona dhahiri
    Mwana naumia moyo, hayo sikuyadiriki.


  3. Zavuma pepo angani, mavumbi macho sioni
    Ya Rabbi Ya Rahmani, nayahitaji ainy
    Duru hii insani, mwana wa kimasikini
    Mwana naumia moyo, hayo sikuyadiriki.


  4. Zaidi ya kumi mara, yaita haisikiki
    Sikio shahidi pera, ukali wake ashiki
    Natamani hiyo mara, tumbo mepata mikiki
    Mwana naumia moyo, hayo sikuyadiriki.


  5. Katu sikuyadiriki, mwana naumia moyo
    Katu sikuyashiriki, sababu ni yako moyo
    Wapi nitayahakiki, yaliyofichwa na moyo
    Moyo walia machozi, macho yaona majonzi.

"CHAMA"

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet