|
|
Naichagua Suluhu
Date: 07 June, 2003
- Nilipotaka shauri, ndugu munisaidie
Kwa kuipata kwaheri, kwa yule nimpendae
Mukasema ni akheri, wala simfikirie
Nijitie ujabari, na moyoni nimtoe
- Lakini nimebaini, sitoweza kumvua
Toka mwangu mtimani, ambamo alichanua
Wala sinao mwilini, haupo kauchukua
Cha kukifanya sioni, Ila kwenda sujudia
Said Paul
|