.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Ngazi Jamani

 

Related links

Jamani Ngazi

Date: 15 April, 2003

  1. Ngazi imekuwa refu, kufika juu bahati.
    nnaipanda kwa safu, bado sijaona bati.
    miaka imesadifu, napanda ni katikati.
    Napanda ni katikati, ngazi imeleta tifu.


  2. Chini nako sikuoni, ngazi ilikoanzia.
    nimekuwa hamkani, nimengia na tanzia.
    juu hakuonekani, na chini kumepotea.
    Na chini kumepotea, hiki ni kioja gani.


  3. Shauri nalishauri,wapi pa kuelekea.
    tena nimetia ari,ari ya kuteketea.
    kuruka juu tayari,au chini kutelea.
    Au chini kutelea,yote mawili jabari.

John Smith

 

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet