.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Chemsha Bongo Mapenzi

 

Related links

CHEMSHA BONGO-MAPENZI

03 Juni, 2003


  1. Pendo lako siliwezi, uzito nanga karuwa
    Linan'gara kama mwezi, kuangalia lauwa
    Mimi kwako mwanagenzi, fani zinanisumbuwa.


  2. Kupenda akupendaye, mithili uwa chanuwa
    Hapo wewe huwa yeye, hakuna la kusumbuwa
    Mwenginewe huwa siye, vigumu kuwabaguwa.


  3. Mapenzi ya kizamani, leo hatunayo tena
    Yanawasha kama weni, na matusi mbayana
    Watamani kujilani, kila kitu chagongana.


  4. Akicheka unanuna, alia wewe waguna
    Mwabaki kudanganyana, nyuma na mbele hakuna
    Wamuona wakazana, na uso unauchuna.


  5. Ukiapizwa kwa pendo, bora upondwe na gari
    Mwendo wako kaa- gando, wendako watahadhari
    Shomari waita dodo, mtoriro ni achari.

Hashil

 


  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet