.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Sudfa

 

 

 

 

 

 

Related links

Sudfa!

Date:  23 Sept 2002

  1. Mwenzako ninawazia, nashindwa kupata jibu
    Ardhi ilipofikia, Waja wameiharibu
    Kila pembe ya dunia, imezongwa na hurubu
    Ndipo ulipotokea, Ukanitunuku hubu
  2. Kwanini tukakutana, katika kipindi hiki
    Watu wamesongomana, kila saa ni mikiki
    Bure wamenuniana, harusini hawacheki
    Ila ninapokuona, huzisahau hilaki
  3. Asubuhi nimechoka, jioni nitaabani
    Kila ninachokishika, hakikai mikononi
    Ni kimoto kinafuka, chavukuta ndani ndani
    Wangu moyo hufunguka, nikutiapo machoni
  4. Chuki na mengi maovu, ndiyo yanayoongoza
    Kila mtu ana kovu, au donda auguza
    Huonekana mwerevu, mambo anoyabiruza
    Bila wako uokovu, singeona muangaza

 

Said Paul

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet