|
|
CHEMSHA BONGO-KWENYE UWANJA WA MASHAIRI
Date: 3 July, 2003
- Kaziye ni kubwabwaja, asemayo hayajuwi
Kuwakuza wasohaja, simashina si matawi
Harufu chenza kangaja, sivipofu si visiwi.
- Kashika kuwasafisha, choo harufu waridi
Kutwa atuhamakisha, kuwa yeye ni shahidi
Nyimbo zake zisokwisha, za tambuu na magadi.
- Twaelezwa yalofanywa, machoni hatuyaoni
Yako tunayoyajuwa, mauwaji ya mitoni
Na heshi kutusumbuwa, nakututia huzuni.
- Yalopita ni mshindo, kusahaulika vigumu
Yalopita kama nyundo, wakumbuka walasumu
Yalopita si magendo, uovu wamwanaadamu.
- Muumba tupe imani, tusahau ya zamani
Tumegeuka manyani, twaninginia mitini
Kutwa tuko vichakani, huu kwetu mtihani.
Hashil S. Hashil
|