.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Yasikutie Uchungu

 

 

 

 

 

 

Related links

Yasikutie Uchungu!

Date:  23 Oct 2002

  1. Sisikitike mwenzangu, hayo mambo ya kupita
    Yasikutie uchungu, ukikaa ukijuta
    Wewe muachiye Mungu, na yeye yatamkuta
    Arudi kukutafuta
  2. Si wote wenye kinaa, kiwapa wakatosheka
    Wengine wana tamaa, kubwa isio semeka
    Huwa kama wenye njaa, roho huwapaparika
    Imani ikawatoka
  3. Huzisahau hisani, roho zikabadilika
    Wakawa mafirauni, kutenda yaso mipaka
    Si kwa siri,majiani, bila haya hufanyika
    Ukiona tashituka
  4. Khofu kwao huwatoka, huhamkwa hadharani
    Kwa kejeli na kucheka, nawe ukawa huoni
    Pale utapo shituka, mali iko kwa jirani
    Hujuwi ufanye nini
  5. Dalili ni tangu mwanzo, mapenzi hakuwa nayo
    Bila ya shaka ni chanzo, chake akawa mchoyo
    Ana mengi matatizo, kwa hali hiyo aliyo
    Wakupenda huyo siyo
  6. Nawe fanya umetupa, kitu kisicho thamani
    Na vyote ulivyompa, vibaidishe moyoni
    Huku siku unazipa, atakutoka yakini
    Atajuwa wewe nani

 

Maher

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet