.

Welcome to Zanzinet Swahili Poems

Where Swahili matters!

Bora Urafiki

 

 

 

 

 

 

Related links

Bora Urafiki!

Date:  04 April 2004

  1. Waonaje, tukabaki marafiki
    Ingawaje, twalingana akhlaki
    Tufanyeje, yeyote halaumiki
    Ni kheri ya haya
  2. Urafiki, yeyote halazimiki
    Kimiliki, kutowa ni yako ashki
    Kiashiki, furahisha halaiki
    Ni kheri ya haya
  3. Twewaona, wapenzi walopendana
    Kishikana, mithili ya ndizi chana
    Metengana, sasa wamenuniana
    Ni kheri ya haya
  4. Usuhuba, lawama waiepuka
    Sio huba, yabidi kulazimika
    Mahabuba, yake radhi kumtaka
    Ni kheri ya haya

 

Chakupewa

  About Us | Zanzinet Home | Contact Us | ©2004 Zanzinet