|
|
Chemsha Bongo
Date: 19 August, 2004
- Wenye nogwa tuko wengi, ukimkwaa kiyama
Hujibadilisha rangi, kinyonga awekwa nyuma
Wala hawavuti bangi, mikasa yao nakama.
- Twendako kuna dharuba, tujizatiti kikweli
Hakuhitaji mahaba, tujifanye ziraili
Maneno yawe ya mimba, muwasho wa pilipili.
- Ccm muflisi, wakijuacho fitina
Nyendo zao kama fisi, wakipatacho wavuna
Wapinzani ni waasi, wao ndio waungwana.
- 2005 songombingo, mwaka huo wangojewa
Hata watokunjwa gongo, akili zawa muruwa
Mwenye macho awa chongo, kumbe anakuchunguwa.
- Mfundoni nimefika, nasubiri zenu hoja
Kijiwe kitakalika, kama twawa ni wamoja
Aduwi kumualika, musifikiri viroja.
Hashil
|