Gombe Dume
Date: 28 Aug 2004
-
Gombe dume limekata - Linazaga mitaani
Lataka leta matata - Wenzangu tahadharini
Popote hupitapita - Laangaza hata ndani
-
Huvila vyakula vyote - Wala si hoja majani
Taka wali na mikate - Hata piya doriani
Fanyeni tulikamate - Tusingiye hasarani
-
Gombe sugu kweli kweli - Hii nawapa yakini
Lapiga na halijali - Litakuja mpaka ndani
Huharibu yote mali - Lateka hata vyumbani
-
Gombe na ujamu wake - Ni mkubwa wa kifani
Wala halina makeke - Bazazi la namba wani
Bora sasa tulisake - Litaleta kisirani
Kiitikio:
-
Gombe dume limekata - Litatutiya hasara
Shairi : Dr. Said Ahmed - Wete - Pemba (1969)
Limeletwa ukumbini na: Saleh M. Barkey